 |
Mshindi wa kinyang'anyiro cha Ubunge katika jimbo la Mtwara mjini anayesubiri kuapishwa, Maftaha Nachuma wa Chama cha Wananchi CUF akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Limbakisye Shimwela.
|
 |
Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo la Mtwara mjini, Limbakisye Shimwela, akitangaza matokeo ya Ubunge yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi
|
 |
Limbakisye Shimwela
|
 |
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Mtwara Mjini, Limbakisye Shimwela, akimkabidhi matokeo ya Ubunge, Mshindi wa jimbo hilo Maftaha Nachuma wa CUF
|
 |
Askari wa Polisi (Field Force) wakiimarisha ulinzi katika eneo la Chuo cha Ualimu Mtwara (TTC) kutokana na wananchi kuwa na shauku ya kutaka kumjua mbunge wao kiasi cha kutaka kuvamia ukumbi wa majumuisho.
|
 |
Wafuasi wa CUF waliokuwa wakisubiri matokeo ya Ubunge jimbo la Mtwara mjini
|
 |
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mtwara mjini, Limbakisye Shimwela, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangaza matokeo ya Ubunge.
|
Na Juma Mohamed
Msimamizi wa
Uchaguzi katika jimbo la Mtwara mjini, Limbakisye Shimwela, amemtangaza mgombea
Ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma, kuwa
ndio mshindi baada ya kuwazidi kwa idadi ya kura wagombea wenzake.
 |
Limbakisye Shimwela
|
Akitangaza matokeo
hayo jana jioni katika kituo cha majumuisho kilichopo katika chuo cha waalimu
Mtwara (TTC), amesema Nachuma aliyekuwa akichuana na wagombea wa vyama vya
ACT,NCCR,CHADEMA na CCM, ameshinda kwa kura 26,655 sawa na asilimia 47.16,
akimzidi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Hasnain Murji aliyepata
kura 24,176 sawa na asilimia 42.78.
 |
Limbakisye Shimwela
|
Akizungumza baada
ya kutangazwa mshindi, Nachuma amesema ameyapokea kwa furaha matokeo hayo na
kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na watu wote bila kujali itikadi za vyama
kwani yeye ni mbunge wa watu wote.
 |
Maftaha Nachuma, akizungumza na waandishi wa habari.
|
Waliojiandikisha
katika jimbo hilo ni 83,837 ambapo waliopiga kura halali ni 56,515 na kwamba
katika kata 18, CCM wamepata kata 7, CUF kata 8 huku kata tatu zikichukuliwa na
CHADEMA.
No comments:
Post a Comment