Msanii wa Filamu, Shamsa Ford. |
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ally Timbulo (Timbulo) |
Na Juma Mohamed
Baadhi ya
wasanii wa filamu na muziki hapa nchini wamesema wamechoshwa na utawala wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanaamini unachangia kurudisha nyuma maendeleo
ya sanaa, na kuamua kuunga mkono upinzani.
Akizungumza
mkoani Mtwara leo, muigizaji maarufu wa filamu, Vicent Kigosi (Ray), amesema nchi
ya Tanzania ina kila aina ya utajiri lakini hauwanufaishi wananchi wake huku
akiwashangaa wasanii wanaounga mkono CCM wakati wanajua hakina faida kwao.
"Tumekuwa tukipewa ahadi nyingi ambazo hazina msingi, na tunashangaa kuna baadhi ya wasanii wanajua shida za wasanii na shida za watanzania wote ambao ni masikini wa kutupwa ambapo nchi hii ina kila aina ya utajiri..kwahiyo nimekuja Mtwara kuwaambia kwanza Mtwara mumepigwa kwenye gesi, kwahiyo watu wa Mtwara badilikeni na mchagueni Lowassa, huu ndio wakati wa madiliko sasa nchi yetu hii.." alisema Ray.
Na kuongeza "Chama Cha Mapinduzi kimekaa madarakani miaka zaidi ya 50 na hawajafanya mabadiliko..sasaivi tunataka mabadiliko, na hata wakisema Lowassa sijui fisadi, tunamtaka huyo huyo fisadi..hatumtaki Magufuli kwasababu CCM tumeshaichoka kukaa katika nchi hii na tunahitaji mabadiliko.." aliongeza.
Naye, msanii
na muandaaji wa muziki wa kizazi kipya, Rahim Ramadhan (Bob Jounior), amesema lengo
la kutembelea mkoani humo ni kuwahamasisha wananchi kuunga mkono vyama
vinavyouna Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutembelea makundi maalumu
ikiwa ni pamoja na watoto yatima.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Fred Marick (Mkoloni) |
Wasanii hao
zaidi ya 30 waliwasili mkoani humo jana na kutumbuiza katika viwanja vya
Mashujaa, ikiwa ni harakati za kumnadi mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) chini ya UKAWA, Mhe. Edward Lowassa na mgombea ubunge wa
Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma.
No comments:
Post a Comment