Mariam Malak |
Jambo la kushangaza ni kwamba, mwanafunzi huyo
amekuwa mfano wa kuigwa nchini humo kutokana na alama za juu alizopata katika
mitihani ya awali, alikuwa na matarajio ya kuzoa alama ya juu zaidi yaani A
itakayomwezesha kujiunga na chuo cha mafunzo ya daktari lakini.
Katika mtihani wake wa mwisho, Malak alipewa alama
za chini zaidi, ikimaanisha kuwa hakuandika hata herufi moja aliyojibu
kikamilifu.
Mariam Malak |
Kutokana na hali hiyo, mwanafunzi huyo anashuku kuwa kulitokea
kosa kubwa kwani yeye alivyofanya mtihani huo hadhani kama angeufeli.
''Kwa kweli sikuamini macho yangu eti nimefeli
mtihani wa mwisho'' alinukuliwa Malak na Shirika la Utangazaji la Nchini
Uingereza (BBC).
Aidha, baada ya kutafuta jina lake bila ya mafanikio katika
orodha ya watahiniwa waliopasi mtihani wao wa mwisho, alipoteza fahamu papo
hapo.
Malak alikuwa hajaufeli mtihani mmoja bali alikuwa
amezoa sufuri katika masomo yote saba.
Yaani alikuwa ameambulia sufuri juu ya mia 0% katika
masomo yote saba.
''Hii sio kweli''
Familia yake inadai kuwa huwenda malaka ameangushwa
mtihani wake wa mwisho maksudi tu kwa sababu ya hila, na kwamba huenda ikawa ni
njama ya kufifisha ndoto yake ya kuwa daktari.
Awali ilidhaniwa kuwa alichukiwa kwa sababu yeye ni
wa kutoka kwenye tabaka la Wamisri wachache ambao ni wakristo wa kicoptic
lakini dhana hio ilikataliwa.
Wizara ya Elimu imelazimika kumpa mtihani wa kubaini
iwapo hati iliyowakilishwa kwa jina lake ni yake haswa ama ni ghushi, hata
hivyo ikatoa uamuzi kuwa ilikuwa yake haswa.
Hata hivyo maelfu ya watu waliotazama nakala za hati
aliyoandika kwenye runinga walisema hazifanani kabisa na zile zilizopewa jina
lake.
Kufuatia tofauti hiyo, ukurasa ulianzishwa kwa nia
ya kuishinikiza wizara ya elimu kuingilia kati kutanzua kitendawaili hicho.
Ukurasa huo unawafuasi takriban 30,000 kufikia sasa.
Tayari watu kadha wamejitokeza kugharamia malipo
yake yote ya chuo kikuu.
Ndugu yake Mina anasema kuwa wanashuku majibu yake
yalipewa mtu mwengine.
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment