Wednesday, April 8, 2015

MILIONI 27 ZAKUSANYWA, USIKU WA V.I.P

Na Juma Mohamed, Mtwara.

Milioni 16 kati ya 27 zilizopatikana katika tamasha la usiku wa V.I.P wiki iliyopita zitagawanywa asilimia 50/50 kwa manispaa ya Mtwara na halmashauri kwa ajili ya kusaidia kutengeneza fenicha za maabara za shule za sekondari za halmashauri hizo.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatuma Ally.

Hayo yamezungumzwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatuma Ally, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyopatikana katika tamasha hilo ambalo lilikuwa ni la aina yake kutokana na burudani safi kutoka kwa bendi ya muziki wa taarab ya Jahazi, ikiongozwa na Mfalme Mzee Yusufu katika ukumbi wa Makonde Beach, mjini hapa.

Alisema lengo limefanikiwa kwasababu faida imepatikana ambayo ni sh. milioni 16, ambapo milioni 11 zimetumika katika gharama za maandalizi ya tamasha na kiasi kingine kuilipa bendi ya Jahazi.

................................mwisho.................................................................

No comments: