![]() | |
| Ndanda Fc |
| Simba Sc |
Na Juma Mohamed
Maandalizi
ya mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Ndanda Fc dhidi ya Simba
inayotarajiwa kufanyika hapo kesho katika uwanja wa Nangwanda Sijaona hapa
mkoani Mtwara, yanakwenda vizuri, huku mechi kamishna na waamuzi wakitarijiwa
kuwasili leo tayari kwa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa wa upinzani wa hali
ya juu, kutokana na timu zote kuwa katika nafasi za chini katika msimamo wa
Ligi hiyo.
Wenyeji
Ndanda Fc wao wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wakiwa na alama 10, huku
wapinzani wao wekundu wa Msimbazi wakiwa katika nafasi ya 12 na alama zao 9.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mtwara, Othmani
Kambi, amesema timu zote mbili tayari zipo hapa mkoani Mtwara na hakuna taarifa
zozote za matatizo kuhusiana na mchezo huo.
Kuhusu
tiketi ni kwamba zinatarajiwa kuanza kuuzwa mapema hapo kesho, ambapo mashabiki
wataingia uwanjani kwa shilingi elfu 5 na shilingi elfu 3.
Aidha Kambi amezungumzia
utaratibu wa kuingia magari uwanjani, kuwa hakutakuwa na gari lolote litakalo
ruhusiwa kuegeshwa ndani ya uwanja, na wametenga sehemu za kuegesha magari nje
ya uwanja ambapo magari yatakayoruhusiwa kuingia ni ya askari polisi, mgeni
rasmi na gari la zima moto
Ikumbukwe
kwamba timu hizi zilikutana katika mchezo wa kirafiki hapa mkoani Mtwara mwaka
jana katika tamasha la Ndanda day, na mchezo kumalizika kwa suluhu.
Simba wao
kabla ya mchezo huu walikuwa wakishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi kule
Zanzibar, ambapo wameibuka mabingwa baada ya kuwafunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju
ya Penalt 4-3, huku Ndanda wakitoka sare ya goli 1-1 na Polisi Moro, katika
mchezo wa Ligi kuu uliofanyika hapa Mkoani Mtwara wiki moja iliyopita.

No comments:
Post a Comment