Wednesday, November 19, 2014

SUNDERLAND NA QPR WAONJA JOTO LA JIWE KUTOKA FA




Na Juma Mohamed

 Sunderland na Queens Park Rangers wamepigwa faini ya £20 000 kila mmoja kwa kushindwa kudhibiti wachezaji wao katika mechi mbili tofauti za Ligi ya Premia, Shirikisho la Soka la Uingereza lilisema Jumatatu.

Klabu zote mbili zilikiri kosa la “kukosa kuhakikisha wachezaji wake wanadumisha nidhamu”, shirikisho hilo linalosimamia soka lilisema kwenye tovuti yake (www.thefa.com).

Faini ya Sunderland inatokana na kisa cha dakika ya 76 wakati wa sare yao ya 1-1 na Everton uwanja wa Stadium of Light Novemba 9.

Wachezaji wa Sunderland walipokea kwa hasira uamuzi wa refa Le Mason wa kuwapa Everton penalty kutokana na kosa la straika wa Sunderland Connor Wickham dhidi ya Seamus Coleman.

QPR waliadhibiwa kutokana na vitendo vya wachezaji wao baada ya uamuzi wa refa Mike Riley wa kumnyima straika wao Charlie Austin mabao mawili – yote dakika ya nane – wakati wa sare yao ya 2-2 na Manchester City Loftus Road Novemba 8.

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: