Wednesday, November 19, 2014

LUKA MODRIC KUKOSA MECHI ZOTE ZA R. MADRID KABLA YA MWAKANI

B2lsnjHCUAEVv4V Real Madrids Luka Modric injured for Croatia v Italy, set to miss 2 3 weeks
Luka Modric
Na Juma Mohamed

Kiungo wa Real Madrid Luka Modric atakosa kipindi kilichosalia cha mwaka huu baada ya kuumia paja, viongozi hao wa La Liga walisema kupitia taarifa Jumatatu.


Modric alitolewa kipindi cha kwanza katika mechi ya Croatia ya kufuzu kwa Euro 2016 nchini Italia baada ya kuumia Jumapili, na wasiwasi wa daktari wa timu Boris Nemec kwamba alipata jeraha litakalomuweka nje kwa zaidi ya mwezi mmoja umethibitishwa.

“Uchunguzi wa matabibu kutoka Real Madrid wamegundua kuna jeraha la misuli guu lake la kushoto,” Real walisema.

Modric, na utoaji pasi safi na kutamba safu ya kati, amekuwa nguzo kuu katika mwanzo mwema wa Real msimu huu ambapo kufikia sasa wanaongoza La Liga na alama 27 kutokana na mechi 11.


SOURCE: SUPER SPORT

No comments: