Tuesday, July 8, 2014

NEYMAR AWE CHACHU YA KUTUFIKISHA FAINALI: SCOLARI

Luiz Felipe Scolari
Na Juma Mohamed

Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari ametoa wito kwa vijana wake watumie kuondoka kwa Neymar kutokana na jeraha kama motisha watakapoikabili Ujerumani katika nusufainali ya Kombe la Dunia Jumanne.
Mchezjai huyo wa miaka 22 atakosa mechi zilizosalia za dimba baada ya kuumia mgongoni wakati wa ushindi wao wa 2-1 katika mechi ya robofainali dhidi ya Colombia.
“Ninadhani motisha zaidi tunaofaa kuwa nao kila mechi ni kuendelea mbele hatua nyingine na kukaribia lengo letu kuu la kufika fainali,” Scolari alisema Jumatatu.
"Jinsi Neymar alizungumzia wachezaji iliwafanya waelewe kwamba amefanya kazi yake na sasa tunafaa kufanya kazi yetu.
“Mimi, na wachezaji wengine, watu wote wa Brazil. Mechi hii ni muhimu, inaweza kutufikisha fainali.
“Tunachezea taifa letu, kila kitu tulichowahi kutafakari na kuota, na pia kwa Neymar.”

Ukali wa Scolari katika kufikisha timu yake nusu fainali umekashifiwa na walifikia kilele kwa kufanya madhambi mara 31 waliopishinda Colombia.
Na meneja huyo wa zamani wa Chelsea alikiri hawajacheza vyema sana vile wangetarajiwa kama wenyeji.
"Tunafanya kila kitu hatua kwa hatua, si kila wakati kwa njia maridadi lakini tunakaribia fainali nyumbani na kwa hivyo kila kitu ni kama tulivyopanga.”

No comments: