Friday, July 4, 2014

Lloris atoa saluti kwa Neuer

Manuel Neuer

Golikipa na nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris alisifu mwenzake upande wa Ujerumani Manuel Neuer kama bora zaidi kabla ya timu hizo kukutana robofainali ya Kombe la Dunia Ijumaa.
Huku walinzi wa Ujerumani wakiingia ndani sana uwanjani ushindi wao wa 16 bora dhidi ya Algeria, Neuer alijikuta akitoka nje sana ya eneo lake kufagia mpira.
Na Lloris alifurahishwa sana na jinsi nyota huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 28 alivyofanya kazi yake kama ‘kipa wa kufagia’.
"Timu inapoingia sana uwanjani, lazima uweze kucheza vyema mbele na kufanya kazi kama 'libero' (mlinzi wa kutanga)," Lloris alisema kabla ya mechi hiyo itakayochezewa uwanja wa Maracana.
"Neuer bila shaka ndiye kipa kamili zaidi duniani na mwenye uwezo wa kutekeleza jukumu hilo. Alifanya hilo vyema sana dhidi ya Algeria."

No comments: