Thursday, March 7, 2013

VIONGOZI WA SIMBA WAANZA KUACHIA NGAZI, BAADA YA POPPE SASA NI KABURU NAE ANG'ATUKA



MJUMBE wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo GEOFREY NYANGE KABURU wamejiuzulu nyadhifa zao katika klabu hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Timu hiyo kuondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika na timu ya LIBOLO ya nchini ANGOLA.


Mapema leo mchana mwandishi wa kituo hiki kwa njia ya simu HANS POPPE amewasilisha barua yake ya kujiuzulu katika klabu hiyo huku akielezea kusitikishwa kwake na hali halisi ndani ya klabu hiyo lakini ameahidi kuendelea kuwa mwanachama wa klabu hiyo.

Kauli ya HANS POPPE imekuja baada ya timu ya SIMBA kuondoshwa katika michuano hiyo mikubwa ya Afrika ambapo aliongozana na timu hiyo kwenda nchini ANGOLA.

Majira ya jioni, taarifa zilizotolewa na msemaji wa SIMBA , EZEKIEL KAMWAGA pia zilithibitisha kuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo GEOFREY NYANGE KABURU naye ameandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo ISMAIL ADEN RAGE ambaye yupo nchini INDIA.

Wakati katika msimamo wa ligi unaonyesha kuwa SIMBA ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 31, sawa na COASTAL UNION ya TANGA

No comments: