Tuesday, March 5, 2013

MAMBO YA KUKUMBUKWA KUELEKEA MECHI YA LEO



KIKOSI CHA MAN UTD

KIKOSI CHA MADRID
KOCHA Sir Alex Ferguson ana rekodi mbaya dhidi ya timu za Jose Mourinho. 
Kocha huyo wa United, ameshinda mechi mbili tu katika 15 dhidi ya Mourinho, ambaye alipata mafanikio akiwa  na klabu za Porto, Chelsea, Inter Milan na sasa Real Madrid. 
Ameshinda mechi sita, ametoa sare saba.

Hapa ni mechi tano za kukumbukwa zaidi baina ya makocha hao...

2004: Porto 2 Manchester United 1
Ligi ya Mabingwa, Uwanja (Estadio) wa (do) Dragao
Baada ya Quinton Fortune kuipa United bao la kuongoza katika mechi hii ya kwanza ya hatua ya 16 bora, Roy Keane alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Benni McCarthy, akafunga mabao mawili kuipa Porto ushindi.

Katika mechi ya marudiano, Paul Scholes aliifungia United bao la kuongoza, lakini Costinha akasawazisha dakika za lala salama.

2005: Manchester United 1 Chelsea 0
Ligi Kuu England, Uwanja wa Old Trafford
Chelsea walitwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu, baada ya miaka 50, miezi sita iliyotangulia, lakini bao la kichwa la Darren Fletcher lilitosha kuwapa ushindi Man U Novemba mwaka huo, kabla ya kikosi cha Mourinho kutetea ubingwa wake Mei.

2007: Chelsea 1 Manchester United 0 (dakika 120)
Fainali Kombe la FA, Uwanja wa Wembley
Wiki mbili baada ya kupokonywa taji la Ligi Kuu England na Man United, Mourinho aliipeleka Chelsea Uwanja wa Wembley, kwa ajili ya fainali ya kwanza kuchezwa kwenye Uwanja huo tangu ukarabatiwe.

Baada ya dakika 90 za bila kufungana, Didier Drogba alifunga bao katika dakika 30 za nyongeza kumpa Mourinho taji hilo mara mbili mfululizo.

2009: Manchester United 2 Inter Milan 0
Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa Old Trafford
Baada ya sare ya bila kufungana, katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Uwanja wa San Siro, mabao ya kichwa ya Nemanja Vidic na Cristiano Ronaldo, yaliivusha hadi Robo Fainali timu ya Ferguson. United ilikwenda hadi Fainali mjini Rome, lakini ikafungwa na Barcelona.

2013: Real Madrid 1 Manchester United 1
Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa Bernabeu
Danny Welbeck aliifungia United, bao la kuongoza kabla ya Ronaldo kusawazisha kwa kichwa baab kubwa. Kipa wa United na mzaliwa wa Jiji la Madrid, David de Gea aliibeba mno timu yake kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari. Leo itakuwaje????? Mimi sijuiiiii…..

No comments: