Wednesday, September 12, 2012

KAMATI YA UTENDAJI YA SIMBA INAKUTANA JONI HII KATIKA HOTELI YA SERENA

  Kutokana na kutoridhishwa na kile kilichoaamuliwa na kamati ya sheria maadili na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini (TFF),juu ya mchezaji Kalvin Yondani,kamati ya utendaji ya Simba jioni hii inakutana katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar Es salaama,kujadiliana juu ya maamuzi yaliyotolewa na kamati ya Mgongolwa.
  Akizungumza na Blog hii muda mfupi uliopita,mwenyekiti wa klabu hiyo Ismaili Aden Rage amesema kwamba, maamuzi yaliyotolewa na kamati ya sheria maadili na hadhi za wachezaji hayakuwa ya haki, na taarifa rasmi juu ya nini kitafanywa na klabu hiyo itatolewa kesho,mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
  Kamati ya sheria maadili na hadhi za wachezaji iliokutana juzi,iliamua pingamizi ambazo zilikuwa zimewekwa na Simba kuhusu wachezaji Mbuyu Twite na Kalvini Yondani kuichezea klabu ya Yanga ya Dar Es salaam.

No comments: