Friday, September 14, 2012

MAANDALIZI YA KUELEKEA TAMASHA LA NGUMI MTWARA YAZIDI KUPETA

  Maandalizi ya tamasha la mchezo wa Ngumi wa kimataifa unaotarajia kufanyika Oktoba 27,mwaka huu Mkoani Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach Club,kati ya bondia kutoka nchini Kenya Patrick Amote na Rashidi Matumla wa Tanzania yanakwenda vizuri,huku mkataba wa pambano hilo ukiwa tayari umekwisha sainiwa.

 













Akizungumza na Safari Radio jana mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo,mratibu wa pambano hilo Mahamud Sinani amesema kwamba,hii leo baadhi ya wawakilishi wa vyombo vya habari vya Dar Es salaam watatembelea katika klabu ya Masumbwi ya Black Mambaz ya Mkoani Mtwara,ili kuona namna ambavyo vijana hao wanajifua kujiandaa na mchezo huo,ambapo baadhi ya mabondia wa klabu hiyo watapanda ulingoni siku hiyo kuonyeshena kazi na mabondia wengine kutoka Dar Es salaam katika mapambano ya utangulizi.

No comments: