Bolton itampa ofa ya
kuendelea kubaki klabuni Fabrice Muamba katika nafasi nyingine, baada ya kiungo
huyo kulazimika kustaafu soka, miezi mitano baada ya kupoteza fahamu uwanjani
kwa tatizo la moyo.
Uamuzi huo ulichukuliwa
baada ya Muamba kuonana na mtaalamu bingwa wa matatizo ya moyo, Pedro Brugada
nchini Ubelgiji wiki iliyopita. Pamoja na hayo, upasiaji wa kusafisha moyo wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ulikwenda vizuri.
Bolton's Fabrice Muamba
alipata mataizo ya moyo Machi, mwaka huu
Muamba (katikati) akiwa
na famili ya klabu katika siku ya kufurahia, Jumapili
Muamba akiwa amebeba
Mwenge wa Olimpiki Waltham Forest
Muamba alipata matatizo
ya moyo Uwanja wa White Hart Lane mwezi Machi
Wachezaji wa Bolton na
Spurs na kocha wa Wanderers, Owen Coyle (katikati),wakimuangali Muamba akipatiwa
huduma ya kwanza
Meseji kibao za kumtakia
kupona haraka Muamba zikiwa zimewekwa katika Uwanja wa Bolton, Uwanja wa Reebok,
wakati alipokuwa hospitali
Dunia ya soka iliungana
kumtumia ujumbe wa kumuombea kupona mapemaMuamba
Muamba na mtaalamu wa
moyo, Dk Andrew Deaner (kushoto) na Mshauri wa masuala ya moyo, Dk Sam Mohiddin,
madaktari ambao waliokoa maisha yake
Muamba akitoa machozi
aliporejea kwenye Uwanja wa Reebok, Mei mwaka huu
Muamba akifuta machozi
Uwanja wa Reebok, Mei mwaka huu
Muamba na mpenzi wake
Shauna baada ya kupona
Muamba alipewa Shahada
ya heshima Chuo Kikuu cha Bolton
Fabrice Muamba: Kutoka Kinshasa hadi Ligi Kuu England
1988: Alizaliwa April 6 mjini Kinshasa, Zaire
(sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).
1999: Alikwenda England akiwa ana umri wa miaka
11, kuungana tena na baba yake ambaye alikimbia vita Kongo.
2002: Alijiunga na timu ya vijana iliyoundwa na
Arsenal - klabu ambayo alikuwa anaishabikia alipokuwa mdogo nyumbani kwao -
kabla ya kuhitimu katika Akademi hiyo miaka miwili baadaye.
2005: Alisaini mkataba na Arsenal na kucheza
mechi mbili za kikosi cha kwanza zote zikiwa za Kombe la Ligi dhidi ya
Sunderland, Oktoba 25.
2006: Agosti alijiunga na Birmingham kwa mkopo
wa muda mrefu na huko alicheza mechi 36 kabla ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora
Chipukizi wa msimu.
2007: Me 11 - Alihamishiwa moja kwa Birmingham
baada ya klabu hiyo kukubali kulipa pauni Milioni 4 Arsenal.
Agosti 21 -
baada ya kuchezea timu zote za vijana za England kuanzia U-16s, Muamba
alichezeshwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha England U-21 dhidi ya Romania,
mechi ya kirafiki.
2008: Juni - Scores alifunga mabao mawili
katika mechi 37 za ligi msimu wa 2007/08, lakini hakuinusuru Birmingham
kushuka.
Agosti 7 -
Alisaini Bolton baada ya Trotters kukubaliana dau la pauni Milioni 5 na
Birmingham kwa ajili ya kiungo huyo.
2010: Agosti 10 - Alisaini mkataba mpya wa
miaka minne Bolton, ambao ungemalizika mwaka 2014.
2011: Juni - aliichezea England U-21 katika
michuano ya Mataifa ya Ulaya nchini Denmark.
Agosti 13 - alifunga bao lake la tatu katika ligi akiwa na Bolton ikiifunga 4-0 QPR.
Agosti 13 - alifunga bao lake la tatu katika ligi akiwa na Bolton ikiifunga 4-0 QPR.
2012: Machi 17 - Muamba alizimia uwanjani
dakika ya 41, Bolton ikicheza mechi ya Kombe la FA naTottenham Uwanja wa White
Hart Line, kabla ya kupelekwa katika hospitali ya London Chest, ambako alitibiwa
hadi kupona.
Agosti 15 -
Anatangaza rasmi kustaafu soka, baada ya kushauriwa na daktari.
No comments:
Post a Comment