Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya
MANCHESTER CITY, MAN UNITED ZAMGOMBEA VAN PERSIE...
NAHODHA wa Arsenal, Robin
van Persie ameamua kutosaini mkataba mpya na klabu yake hiyo na kwa sababu hiyo
anaweza kufuata mshahara bwa pauni 220,000 kwa wiki katika klabu bingwa England,
Manchester City.
KLABU
ya Manchester United nayo imeonyesha nia ya kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu
ya England, Robin Van Persie, Mholanzi mwenye umri wa miaka 28 na wana matumaini
makubwa watamdondoshea Old Trafford.
Mark
Hateley amemtaka mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka
23, kuondoka Liverpool na kujiunga na AC Milan, akisema kwamba kwa kufanya hivyo
atakuwa mchezaji babu kubwa zaidi.
NYOTA
wa Italia, Andrea Pirlo amemtaka mshambuliaji, Mario Balotelli, mwenye umri wa
miaka 21, kujiunga naye katika klabu ya Juventus, baada ya kusema kwamba sasa
anajua namna ya kumchezesha mchezaji huyo wa Manchester City ili apige mabao
lukuki.
KLABU
ya Sunderland imejiunga katika mbio za kuwania saini ya nyota wa Ajax, Vurnon
Anita, kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uholanzi. Newcastle tayari imeweka
dau la pauni Milioni 4.5 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23,
lakini likapigwa chini.
NYOTA
wa zamani wa Real Madrid, Guti, mwenye umri wa miaka 35, anafanya mazoezi na
West Ham kuelekea kujiunga nayo kama mchezaji huru.
KLABU
ya Benfica inamfukuzia kiungo wa Manchester United, Anderson, mwenye umri wa
miaka 24, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ureno.
KLABU
ya Newcastle United ipo karibu kuinasa saini ya beki wa kulia wa Lille ya
Ufaransa, Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 26, licha ya Inter Milan ya
Italia nayo kutuopa ndoana zake.
KLABU
ya Fulham ipo tayari kumsaini kipa wa Blackburn, Paul Robinson, mwenye umri wa
miaka 32, baada ya mpango wake wa kuhamia Besiktas kudunda.
DI MATTEO ATETEA BASI LAKE CHELSEA
KOCHA
wa Chelsea, Roberto Di Matteo amesema ni makosa kuisema timu yake inakosea kwa
staili yake ya kucheza kwa kupaki basi kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya
dhidi ya Barcelona katika Nusu Fainali na Bayern Munich katika fainali, ambazo
zote walishinda na kutwaa ubingwa.
ARBEOLA APAGAWA...
BEKI
wa Hispania, Alvaro Arbeloa alikuwa mwenye furaha kubwa mno wakati wa
kushangilia ubingwa wa Euro 2012 na mashabiki nchini humo, kiasi cha kufikia
kuruka kutoka kwneye basi
No comments:
Post a Comment