Tuesday, July 10, 2012

ANGALIA KALENDA YA MSIMU YA TFF

ANGALIA KALENDA YA MSIMU YA TFF

Taifa Stars wakipasha

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
KALENDA YA MATUKIO 2012-13
TUKIO TAREHE
KIPINDI CHA KWANZA CHA MATAYARISHO YA MSIMU 01 JUNI HADI 20 AGOSTI 2012
KIPINDI KIKUU CHA MAPUMZIKO KWA WACHEZAJI 01 JUNI HADI 30 JUNI 2012
KIPINDI CHA KWANZA CHA UHAMISHO 15 JUNI HADI 30 JULAI 2012
KUTANGAZA WACHEZAJI WA KUACHWA (SIO WA LIGI KUU) 15 JUNI HADI 30 JUNI 2012
KUTANGAZA WACHEZAJI WATAKAOSITISHA MIKATABA 15 JUNI HADI 30 JUNI 2012
USAJILI WA KWANZA 15 JUNI HADI 10 AGOSTI 2012
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI 11 AGOSTI HADI 18 AGOSTI 2012
KUTHIBITISHA USAJILI HATUA YA AWALI 19 AGOSTI HADI 20 AGOSTI 2012
USAJILI HATUA YA PILI 21 AGOSTI HADI 4 SEPTEMBA 2012
KUTHIBITISHA USAJILI HATUA YA PILI 5 SEPTEMBA HADI 6 SEPTEMBA 2012
KUTAYARISHA TIMU KIPINDI CHA KWANZA 01 JULAI HADI 20 AGOSTI 2012
MECHI ZA KIRAFIKI ZIARA NDANI NA NJE YA NCHI 01 JULAI HADI 20 AGOSTI 2012
KUTOA RATIBA YA LIGI KUU 23 JULAI 2012
KIPINDI CHA KWANZA CHA MASHINDANO 25 AGOSTI HADI 04 NOVEMBA 2011
NGAO YA HISANI KUCHEZWA MIKOA YOTE KUFUNGUA MSIMU 25 AGOSTI 2012
LIGI KUU YA VODACOM MZUNGUKO WA KWANZA KUANZA 01 SEPTEMBA 2012
LIGI DARAJA LA KWANZA -NYUMBANI NA UGENINI KUANZA 15 SEPTEMBA HADI 04 NOVEMBA 2012
LIGI YA TAIFA
NGAZI YA WILAYA KUANZA - MIKOA YOTE 08 SEPTEMBA HADI 31 OKTOBA 2012
LIGI YA WANAWAKE
NGAZI YA WILAYA KUANZA - MIKOA YOTE 08 SEPTEMBA HADI 31 OKTOBA 2012
KOMBE LA FA
HATUA YA AWALI - NGAZI YA WILAYA NA MKOA 24 SEPTEMBA 2012 HADI 12 MEI 2013
MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA VILABU
KAGAME CUP JULY 2012.
MASHINDANO YA CAF YA LIGI YA MABINGWA JUL, AUG, SEPT, OCT, NOV,DEC, 2012
MASHINDANO YA KOMBE LA CAF JUL, AUG, SEPT, OCT, NOV, DEC, 2012
MICHEZO YA KIRAFIKI NA MASHINDANO YA TIMU ZA TAIFA
MCHEZO WA KIRAFIKI (TAREHE YA FIFA) AUG, NOV, 2012
MASHINDANO YA CAF/FIFA (TAIFA STARS) JUNI, SEP, OKT,2012
MASHINDANO YA KUFUZU FAINALI ZA CHAN SEPT, OKT, 2012
MASHINDANO CAF YA KUFUZU FAINALI ZA WANAWAKE JUNI, 2012
MASHINDANO YA KUFUZU FAINALI ZA AFCON JUNI, AOG, SEPT, OKT, 2012
MASHINDANO YA CAF KUFUZU FAINALI ZA U.20 JUNI, JULAI, SEPT, 2012
MASHINDANO YA CAF KUFUZU FAINALI ZA U.17 SEPT, OKT, 2012
CECAFA KARUME CUP U.20
CECAFA CUP U.17 AGUSTI, 2012
CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP NOVEMBA, DESEMBA 2012 -KENYA
FAINALI ZA WANAWAKE SEPTEMBA 2012 - EQUATORIAL GUINE
MASHINDANO MENGINE
KOMBE LA KILIMANJARO LAGER (TBL) 23 JULAI HADI 06 AUGOSTI 2012
KOMBE LA BANK ABC 01 AGOSTI HADI 19 AGOSTI 2012
SHIMUTA NOVEMBA 2012
SHIMIWI OKTOBA 2012
MASHINDANO YA VIJANA - U.14
NGAZI YA WILAYA NA MKOA - MIKOA YOTE NOVEMBA NA DESEMBA 2012
MSHINDANO YA TAYSA
MASHINDANO KUFANYIKA NOVEMBA -DESEMBA 2012
MASHINDANO YA SHULE - VYUO
MASHINDANO YA UMISHUMTA
MASHINDANO YA UMISETA JUNI, 2012
MASHINDANO YA SHIMIVUTA DESEMBA 2012
LIGI YA VIJANA WA LIGI KUU YA VODACOM U.20
LIGI YA VIJANA KUCHEZWA 10 NOVEMBA HADI 25 NOVEMBA 2012
KIPINDI KIFUPI CHA MAPUMZIKO 15 NOVEMBA HADI 15 NOVEMBA 2012
TUKIO TAREHE
KIPINDI CHA PILI CHA MATAYARISHO YA MSIMU- 01 DESEMBA 2012 HADI 10 JANUARI 2013
KIPINDI CHA PILI CHA UHAMISHO 15 NOVEMBA HADI 30 NOVEMBA 2012
KIPINDI CHA PILI CHA USAJILI 15 NOVEMBA HADI 15 DESEMBA 2012
KUTANGAZA WACHEZAJI WA KUACHWA (SIO WA LIGI KUU) 15 NOVEMBA HADI 22 NOVEMBA 2012
KUTANGAZA WACHEZAJI WATAKAOSITISHA MIKATABA 15 NOVEMBA HADI 22 NOVEMBA 2012
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI 16 DESEMBA HADI 23 DESEMBA 2012
KUTHIBITISHA USAJILI 27 DESEMBA HADI 28 DESEMBA 2012
KUTAYARISHA TIMU KIPINDI CHA PILI 01 DESEMBA 2012 HADI 31 DESEMBA 2012
MECHI ZA KIRAFIKI ZIARA NDANI NA NJE YA NCHI 01 DESEMBA 2012 HADI 12 JANUARI 2012
KIPINDI CHA PILI CHA MASHINDANO - 01 JAUNARI HADI 31 MEI 2013
KOMBE LA MAPINDUZI 05 JANUARI HADI 12 JANUARI 2013
LIGI KUU YA VODACOM MZUNGUKO WA PILI KUANZA 19 JANUARI HADI 28 APRILI 2013
LIGI DARAJA LA KWANZA (FAINALI) KUCHEZWA 26 JANUARY HADI 16 MARCH 2013
LIGI YA TAIFA
NGAZI YA MKOA KUCHEZWA 05 JANUARI HADI 20 FEBRUARI 2013
NGAZI YA KANDA KUCHEZWA 01 MACHI HADI 25 MACHI 2013
LIGI YA WANAWAKE
NGAZI YA MKOA KWA MIKOA YOTE KUCHEZWA 15 NOVEMBA HADI 20 DESEMBA 2012
NGAZI YA TAIFA KUCHEZWA 26 JANUARI HADI 24 FEBRUARY 2013
COPA COCACOLA
USAMBAZAJI WA FOMU NA USAJILI 01 JANUARI HADI 30 JANUARI 2013
MASHINDANO NGAZI YA WILAYA KUCHEZWA 05 FEBRUARI HADI 30 MACHI 2013
MASHINDANO NGAZI YA MKOA KUCHEZWA 15 APRIL HADI 30 APRIL 2013
KUANDAA TIMU KWA AJILI YA FAINALI YA TAIFA 05 MEI HADI 30 MEI 2013
KOMBE LA FA
FAINALI ZA KOMBE LA FA 12 MEI 2013
MASHINDANO MENGINE
MASHINDANO YA MAJESHI MACHI 2013
MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA VILABU
MASHINDANO YA KOMBE LA CAF FEB, MARCH, APRIL 2013
MASHINDANO YA CAF YA LIGI YA MABINGWA FEB, MARCH, APRIL 2013
CECAFA KAGAME CUP JULY, 2013
KOMBE LA TAIFA
MASHINDANO NGAZI YA MKOA KUCHEZWA 05 APRILI HADI 20 APRILI 2013
MATAYARISHO YA KWANZA YA TIMU YA MKOA 22 APRILI HADI 04 MEI 2013
KUWASILISHA USAJILI WA TIMU YA MKOA-TFF 27 APRILI 2013
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI 29 APRILI HADI 05 MEI 2013
KUPITISHA USAJILI 05 MEI 2013
MASHINDANO NGAZI YA TAIFA- MAKUNDI 05 MEI HADI 12 MEI 2013
MATAYARISHO YA PILI YA TIMU YA MKOA 13 MEI HADI 18 MEI 2013
FAINALI NGAZI YA TAIFA 21 MEI HADI 27 MEI 2013
MICHEZO YA KIRAFIKI NA MASHINDANO YA TIMU ZA TAIFA
MCHEZO WA KIRAFIKI (TAREHE YA FIFA) FEB, 2013
MASHINDANO YA CAF/FIFA (TAIFA STARS) MARCH, 2013

TFF YATOA ANGALIZO, MWONGOZO, UFAFANUZI UCHAGUZI YANGA


<!--[if !vml]-->
<!--[endif]--><!--[if !mso]-->
<!--[endif]-->
Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA

Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shauri Moyo Road
P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815
E-mail: tfftz@yahoo.com . Email: www.tfftanzania.com
<!--[if !mso]-->
<!--[endif]--><!--[if !mso & !vml]--> <!--[endif]--><!--[if !vml]-->
<!--[endif]-->
<!--[if !vml]--><!--[endif]--><!--[if !vml]-->
<!--[endif]-->






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU UCHAGUZI WA KUJAZA NAFASI ZA UONGOZI WA KLABU YA YANGA

10 JULAI 2012

Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa kuzingatia majukumu yake ya kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya TFF, Ibara ya 49 (1), na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga:

<!--[if !supportLists]-->1. <!--[endif]-->Wanachama wote wa TFF, ikiwa ni pamoja na Klabu ya Yanga, wanatakiwa kuzingatia kikamilifu Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF katika kuendesha shughuli zote za uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->2. <!--[endif]-->Wagombea uongozi wote wa wanachama wa TFF wanapaswa kutimiza masharti ya uongozi yaliyoanishwa katika Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->3. <!--[endif]-->Kamati za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinapaswa kutimiza kikamilifu majukumu yao ya kulinda Katiba za wanachama wa TFF na kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF katika michakato ya uchaguzi. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilishaelekezwa kufanya hivyo na inakumbushwa kuendelea kuzingatia wajibu huo.
<!--[if !supportLists]-->4. <!--[endif]-->Wagombea uongozi wa wanachama wa TFF wanao wajibu wa kuzifahamu Katiba zao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kuomba uongozi kwa kutimiza matakwa ya Katiba na Kanuni za Uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->5. <!--[endif]-->Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea maombi ya marejeo (review) dhidi ya uamuzi wake wa kuwaondoa waombaji uongozi wanne (4) wa Klabu ya Yanga. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatoa uamuzi ufuatao:
<!--[if !supportLists]-->i) <!--[endif]-->Marejeo yaliyoombwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga yanakiuka Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeyakataa. Kamati inafafanua kuwa hata kama Kanuni zingekuwa zinaruhusu kufanya marejeo, bado maombi hayo yasingepaswa kuwasilishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, bali waombaji uongozi wenyewe. Pamoja na hayo, sababu za kuomba marejeo si za msingi kwa kuwa waombaji uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga walipewa mwongozo wa kutosha kurekebisha upungufu uliojitokeza katika mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga.

<!--[if !supportLists]-->ii) <!--[endif]-->Sara Ramadhani hakutimiza masharti ya kuomba uongozi kwa mujibu wa Ibara ya 10(4) na (5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kama ilivyoanishwa kwenye Fomu namba 1 kwa kutojaza fomu na kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za kugombea. Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuliondoa jina lake katika orodha ya wagombea uenyekikiti wa Klabu ya Yanga.
<!--[if !supportLists]-->iii) <!--[endif]-->Shaaban R. Katwila na Ahmed Waziri Gao wameshindwa kutimiza masharti ya uombaji uongozi kwa kutowasilisha vyeti halisi kwa ajili ya uhakiki kama ilivyotakiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya nakala za vyeti vyao kubainika na NECTA kuwa vina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutekeleza uamuzi wa kuondoa majina yao kwenye orodha ya wagombea uongozi wa Yanga.
<!--[if !supportLists]-->iv) <!--[endif]-->Ramadhan Mzimba Kampira ameshindwa kutimiza masharti ya kugombea uongozi kama yalivyo kwenye Ibara ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF kwa kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za mgombea. Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuondoa jina lake katika orodha ya wagombea uongozi.
<!--[if !supportLists]-->v) <!--[endif]-->Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaridhia uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga kuwaondoa wafuatao kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi:
<!--[if !supportLists]-->(a) <!--[endif]-->Ally Mayay Tembele
<!--[if !supportLists]-->(b) <!--[endif]-->Abdallah Sharia Ameir
<!--[if !supportLists]-->(c) <!--[endif]-->Jamal Hamisi Kisongo
<!--[if !supportLists]-->(d) <!--[endif]-->Mohamed R Mbaraka

<!--[if !supportLists]-->vi) <!--[endif]-->Wagombea uongozi ambao hawakutajwa hapo juu na ambao walipitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, wametimiza matakwa ya awali ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na hatua za mwisho za uhakiki wa vyeti vya elimu yao, zinaendelea.




Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI TFF

TFF YAPATA MSIBA MWINGINE


Na Prince Akbar
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mara (FAM), Fabian Samo kilichotokea leo asubuhi (Julai 10 mwaka huu).
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura Mgoyo, ameaimbia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, Samo ambaye Novemba 13 mwaka jana alichaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa FAM katika uchaguzi uliofanyika wilayani Rorya alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya figo.
Wambura amesema taratibu za mazishi ya Samo ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu (Internal Audit Committee) ya TFF ikiwemo siku atakayozikwa bado zinafanywa na familia yake.
Amesema Samo alitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Mara na Tanzania kwa ujumla, vitu ambavyo vilichangia kuchaguliwa kwake tena kuiongoza FAM.
Amesema msiba huo ni pigo kwa familia ya Samo, FAM, TFF na mchezo wa mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa kipindi chote alichokuwa kiongozi.
Amesema TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Samo, FAM, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu Samo mahali pema peponi. Amina
Wakati huo huo: Wambura amesema kwamba, wakati wa mechi za Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu, screen kubwa iliyoko uwanjani itatumika kwa matangazo ya biashara na ujumbe mbalimbali kwa washabiki watakaoshuhudia mechi hizo.
Amesema TFF inakaribisha kampuni na wadau mbalimbali wanaotaka kuweka matangazo yao wakati wa michuano hiyo itakayoshirikisha klabu kumi na moja kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Amesema muda wa kurushwa matangazo hayo yanayotakiwa kuwa kwenye mfumo wa DVD ni kabla ya mechi kuanza, wakati wa mapumziko na baada ya mechi. Matangazo hayo yanatakiwa kuwa ya sekunde 60 (dakika moja) au sekunde 30 (nusu dakika).
Aidha, Wambura amesema kwamba Kozi ya makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza leo (Julai 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.
Amesema Wakufunzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ndiyo wanaoendesha kozi hiyo iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Amesema Kozi hiyo itakayomalizika Julai 15 mwaka huu inashirikisha washiriki 35, na mwendelezo wa ile ya awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Amemtaja Gouinden Thandoo kutoka Mauritius ni mmoja wa wakufunzi wa FIFA wanaoendesha kozi hiyo

No comments: