Sunday, June 3, 2012

VIDEO: IVORY COAST 2:0 TANZANIA.


CELEBS BATTLE: DIAMOND VS BOB JUNIOR

alt
DIAMOND PLATNUMZ
1: Who's the best artist between you and Bob Junior?

Everbody knows that Diamond ni hatari kuanzia kimashairi, kuimba, mpaka kwenye performance, that's why kila siku napiga show nje kuanzia Italy, Sweden, Holland, na Greece.Mkata viuno cant touch this milele.
2: Unadhani Bob Junior asingekuwa mwanamuziki angekuwa nani?
Haihitaji kuongea sana kuhusu hili, kutokana na kujua kukatika kama Fifi Moto, basi ningemuajiri kama mcheza shoo wangu.
3: Nani anamiliki mtoto mkali?
My galfriend is best thing that Bob Junior will never have, hivyo sihitaji hata kusema zaidi nisije nikakufuru bure.
4: Which one is the best "Wasafi" or "Sharobaro"?
Wasafi ndio kila kitu, tunajua kupendeza, kutafuta mkwanja na ndio maana tuna maendeleo.What's hell is Sharobaro?
5: Kwa mitupio nani anamuongoza mwenzie?
We mimi noma, wajanja wa town wanakoma na pamba zangu, Sharobaro atabaki kuwa Junior kwenye suala hili and i'll alwayz be his senior.
6: Out of 10, unampa ngapi Bob Junior kama mwanamuziki?
Nafikiri tatu zitamtosha kabisa.
7: Imagine upo ulingoni na Bob Junior, Shabaro angedumu kwa round ngapi?
Round ya kwanza hamalizi, nitampiga kwa KO kali hadi madokta wa hospitali waombe PF3 ya IGP Mwema.
8: Nafasi ya kumshauri Bob Junior hii hapa, unamshauri nini?
Aongeze juhudi katika uproduyza, na akubaliane na ukweli muziki wa Diamond ni platnum, hivyo asijaribu kushindana nao.
alt
BOB JUNIOR
1: Nani msanii mkali kati yako wewe na Diamond?

Mimi ni zaidi ya msanii, najua kuimba, kucheza, napigwa karibia vyombo vyote vya muziki.Mimi ni mwanamuziki niliyekamilika Diamond yupo nyuma sana.
2:Diamond angekuwa msanii, kazi gani nyingine ingemfaa?
Udalali ungemfaa sana, kwani alishawahi kunikodishia watu Coaster nzima waje kwenye show kunizomea Billz.
3: Between you two nani ana demu mkali?
Demu wangu is the finest chick in town, kuanzia reception, figure, mpaka maadili sidhani kama demu wa Diamond ana sifa hizi.
4: Nani anatisha kati ya "Wasafi" na "Masharobaro"?
Masharobaro we are best in town kwa sasa, tumethibitisha kwa mambo mengi ikiwemo kumtoa Diamond kimuziki.Masharobaro a.k.a Mashombeshombe ni hatari.
5:Kwa kunyuka pamba nani anamfunika mwenzie?
Mimi ni raisi wa masharobaro, wasafi na watanashati duniani, Do you think Diamond anaweza kugusa huu moto? aaah you cant be serious¡¡¡¡¡¡¡¡¡¡.
6: How would you rate Diamond out of 10/10?
Nawaachia fans wamchagulie ngapi apewe chini ya namba 4.
7: In the ring wewe na Diamond, nani angeibuka mshindi?
Sekunde 10 za raundi ya kwanza pambano limeisha, maana nitapiga upper cut chini ya kidevu, mtoto wa Tandale chaliiiii.
8: Unapewa nafasi ya kumshauri Diamond, unamwambia nini?
Aende shule akajifunze muziki, ili aweze japo kufikia robo ya level yangu.

Saturday, June 2, 2012

EURO COUNTDOWN: BALOTELLI NA WENZIE WAGONGWA 3-0 NA AKINA ARSHAVIN


Russia 3-0 Italy (Friendly) by goalsarena2012-3

BREAKING NEWS: FLOYD MAYWEATHER AANZA KIFUNGO CHA MIEZI 3 - 50 CENT AMSINDIKIZA JELA

Bondia Floyd Mayweather leo ameanza kifungo cha miezi 3 jela alichohukumiwa mwezi Desemba mwaka jana kutokana na kuvunja sheria kwa kufanya ugomvi. Wakati akielekea Jela Mayweather alisindikizwa na rafiki yake kipenzi mwanamuziki 50 Cent.
Mayweather akitiwa pingu na polisi kuelekea kwenye karandinga.
"Nenda dogo nitakumiss kaka yako" 50 Cent na Mayweather.
Hiki ndio chumba atakachokaa Mayweather kwa miezi 3
Hizi ndio sare zake kwa kipindi chote atakachokaa jela.

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 0 - 2 IVORY COAST FULL TIME



DK 90: Ivory Coast 2-0 Tanzania
DK 86: Goaaaaaaaal Ivory Coast wanapata bao la pili na si mwingine ni Didier Drogba.
DK 80: Kipindi cha pili kinaelekea mwishoni na bado Tembo wanaoongoza kwa bao 1-0
DK 75: Matokeo bado ni 1-0, Ivory Coast wanaongoza.
DK 70: Aggrey Morris anapata kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
DK 68: Ivory Coast 1-0 Tanzania
DK 60: Ivory Coast 1-0 Tanzania
Second Half: Kipindi cha pili kimeanza
Half Time: Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK 43: Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK: 24 - Solomon Kalou anaipatia goli la kuongoza Ivory Coast



Kocha Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)

No comments: