Tetesi za J'pili magazeti Ulaya

FERGUSON APEWA BEI CHAFU KUWANASA MODRIC, TIOTE, BAINES

KOCHA Sir Alex Ferguson ameambiwa kwamba Manchester United itatakiwa kulipa jumla ya pauni Milioni 72 ili kuwapata wachezaji watatu inayowataka - lakini hayuko tayari kutoa fungu hilo kwa ajili ya nyota hao, Luka Modric, mwenye wa miaka 26 wa Tottenham, Leighton Baines mwenye umri wa miaka 27 wa Everton na Cheick Tiote mwenye umri wa miaka 25 wa Newscastle.
KLABU ya Manchester United imemlenga nyota wa Valencia, Jordi Alba, mwenye umri wa miaka 23, kwa kutoa fedha na mchezaji ili kumnasa nyota huyo na mchezaji watakayemtoa atakuwa Mbrazil, Anderson.
KUTOKA kwa mchezaji maarufu wa Liverpool, mshambuliaji Dirk Kuyt, mwenye umri wa miaka 31, inaweza kuwa sehemu ya mpango wa kubadilishana wachezaji na Fiorentina, na beki wa pembeni mwenye thamani ya pauni Milioni 12, Juan Manuel Vargas, mwenye umri wa miaka 28.
Juan Manuel Vargas
Juan Manuel Vargas
KLABU ya Manchester City itaanza kumwaga fedha za usajili kwa ajili ya msimu ujao kwa kutoa pauni Milioni 25 kumnasa beki wa ­Athletic Bilbao, mwenye umri wa miaka 23, Javier Martinez.
TAARIFA za vyombo vya habari nchini Hispania, zimesema Tottenham imepiga hatua ya mawasiliano rasmi ya kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao, mwenye umri wa miaka 27, Fernando Llorente.
KLABU ya QPR inajipanga kumpa ofa kipa wa Tottenham, Heurelho Gomes, mwenye umri wa miaka 31, ili akafufue makali yake Loftus Road.
KLABU ya Arsenal ina nia ya kumsajili mshambuliaji kinda wa miaka 18 wa Crewe mwenye thamani ya pauni Milioni 10, Nick Powell.
KLABU ya Southampton imetenga dau la pauni Milioni 2 kumnasa kiungo wa Millwall, Liam Trotter mwenye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia Fulham na Sunderland.

REDKNAPP MAMBO MAGUMU

MWENYEKITI wa Tottenham, Daniel Levy amekataa kumuongezea mkataba kocha Harry Redknapp, ambaye alitaka apewe miaka mitatu zaidi katika mkataba wake uliobakiza mwaka mmoja na ongezeko la maslahi yake. Hii inamaanisha wawili hao watafanya kazi kwa mgogoro mkubwa msimu ujao.
KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers mpango wake wa muda mrefu ni kutwaa taji na klabu hiyo, akisema; "Yanaweza kuwa manne".
BEKI wa Manchester United, Nemanja Vidic amepewa ruhusa ya kuanza mazoezi kamili mwanzoni mwa mwezi ujao.