Sunday, June 24, 2012

PREVIEW ENGLAND NA ITALIA LEO


Mario Balotelli - Italy
Wachezaji wa Italia
Getty Images
VIKOSI VYA LEO...

ENGLAND

Hart
Johnson, Terry, Lescott, Cole
Milner, Gerrard, Parker, Young
Rooney, Welbeck

ITALIA


Buffon
Abate, Barzagli, Bonucci, Balzaretti
De Rossi, Pirlo, Marchisio
Montolivo
Balotelli, Cassano


BAADA ya kushinda mechi mbili mfululizo, England na kuongoza Kundi D, England leo ikiongozwa na Wayne Rooney itasaka tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya Euro 2012 kwa kumenyana na Italia.

Winga Ashley Young anaelekea kuwa fiti baada ya kuwa majeruhi, hivyo kocha Roy Hodgson anatarajiwa kuanza na kikosi kile kile kilichocheza mechi iliyopita mjini Donetsk, huku Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain wakiwa na matumaini ya kuchukua nafasi ya James Milner katika wingi ya kulia.

Nyuma, beki Glen Johnson anaendelea na matibabu kwa dawa za kuua sumu kwenye kidole cha mguu, lakini hiyo haitamfanya akose mechi ya leo.

Kwa upande mwingine, kocha wa Italia, Cesare Prandelli anatarajiwa kuendelea na mfumo wake wa 4-3-1-2 uliompa ushindi dhidi ya Ireland kuliko mfumo wa 3-5-2 uliomfanya akatoa sare na Hispania na Croatia.

Pamoja na hayo, atamuacha benchi beki wa kati Giorgio Chiellini, ambaye ni majeruhi aliyeumia katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland na sasa anaweza kukosa mechi zote zilizobaki kama The Azzurri itasonga mbele.

Thiago Motta naye yuko shakani kucheza, kutokana na maumivu ya misuli na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Alessandro Diamanti au Riccardo Montolivo.

Mbele, Mario Balotelli anaweza kuanza ili apambane na wachezaji wenzake wa Manchester City, akichukua nafasi ya Antonio Di Natale kucheza pamoja na Antonio Cassano, baada ya kufunga bao katika mechi iliyopita.

Hakuna mchezaji anayetumikia adhabu, lakini Ashley Cole, Steven Gerrard, Milner, Oxlade-Chamberlain, and Young (wote England) na Balotelli, Federico Balzaretti, Leonardo Bonucci, Daniele De Rossi, Christian Maggio, Montolivo, Thiago Motta and Gianluigi Buffon (wote Italia) wamebakiza kadi moja mojqa za njano ili kukosa Nusu Fainali.

JE WAJUA?
  • England imeshinda mechi moja tu katika mechi tisa zilizopita walizokutana na Italia na rekodi ya jumla ya kushinda mechi 6, sare 7 na kufungwa 9 dhidi ya Azzuri.
  • Bao la ushindi la Rooney dhidi ya Ukraine lilikuwa bao lake la 29 anaifungia timu yake ya taifa na anahitaji bao moja zaidi, ili kushika nafasi ya tano katika wafungaji wa kihistoria wa nchi hiyo, akiungana na Tom Finney, Nat Lofthouse na Alan Shearer.
  • Beki wa kushoto, Cole anashikilia rekodi ya kuichezea mechi nyingi England bila kufunga bao, amecheza mechi 97 hadi sasa.
  • Three Lions ilikuwa moja kati ya timu mbili (nyingine Ugiriki) katika hatua ya makundi kucheza bila kuotea kwenye lango la wapinzani.
  • Italy iliifunga England 2-1 katika Kombe la Dunia mwaka 1990 katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
  • Antonio Di Natale ndiye mchezaji aliyeifungia Italia mabao mengi (11) katika kikosi cha sasa Antonio Cassano, Daniele De Rossi, na Andrea Pirlo wote kila mmoja amefunga mabao 10.
  • Katika Robo Fainali kwenye mashindano makubwa, Italia imetolewa katika michuano miwili tu kati ya tisa, na yote kwa mikwaju ya penalti.
  • Prandelli hajashindwa mechi ya mashindano tangu aanze kazi Italia, akiwa ameshinda mechi tisa na kutoa sare nne tangu apewe timu mwaka 2010.

 

Saturday, June 23, 2012

NDONDI FRIENDS CORNER LEO MASHALI NA SAMSON MAWE


Mashali kushoto na Samson kulia baada ya kupima uzito jana

Na Princess Asia
MABONDIA Thomas Mashali na Maisha Samson wanapanda ulingoni leo katika ukumbi wa ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese katika pambano la ubingwa wa Taifa, uzito wa Middle, unaotambuliwa na Chama cha Ngumi (TPBO) chini ya rais wake, Yassin Abdallah.
Mabondia hao jana walipima uzito na wote wakapata kilogramu stahili 71 tayari kwa pambano hilo la raundi 10.
Mbali na pambano hilo, kutakuwa mapambano ya utangulizi kati ya
Juma Fundi na Shaaban Madilu, Mohamed Shaaban 'Ndonga' na Mussa Hassan, Jonas Godfrey na Venance Mponji, Abdallah Mohamed 'Prince Naseem' na Yohana Mathayo raundi sita kila pambano, Nassor Hatibu na Abdul Athuman, Martin Richard na Hassan Kadenge, raundi nne kila pambano

No comments: