Monday, June 25, 2012

ANAYEJUA ANAJUA: DAVID TREZEGUET APIGA 2 NA KUIRUDISHA RIVER PLATE LIGI KUU YA AREGNTINA

Wakati Ufaransa ikitolewa na Spain hatua ya robo fainali ya michuano Ya EURO 2012, mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa mwenye asili ya Argentina David Sergio Trezequet alikuwa ni mwenye furaha baada ya kufunga mabao mawili yaliyoisaidia timu yake ya nyumbani na mabingwa wa zamani wa Argentina River Plate kuweza kupanda daraja na kurudi tena kwenye Ligi Kuu ya Argentina Maarufu Kama Primera A Nacional.

Rive Plate itacheza Primera A Nacional msimu ujao, baada ya kuifunga timu ya Almirante Brown mabao 2-0 na Kufanikiwa kuongoza na kuchukua ubingwa wa Primera B Nacional (Ligi Daraja la pili ya Argentina)
River Plate kwa mshangao mkubwa wa wengi msimu uliopita waliporomoka na kushuka daraja hadi Primera B Nacional baada ya kuwa na msimu mbaya na kufungwa katika mechi ya mwisho ya kuwania kushuka daraja.
Sasa Wamepanda na kurudi tena kwenye ligi kuu ya Argentina Primera A Nacional baada ya msimu moja tu tangu washuke daraja.
River Plate wamepanda daraja pamoja na timu ya Quilmes.

EXCLUSIVE: HIVI NDIVYO MASHABIKI WA CHELSEA TANZANIA WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WA ULAYA











No comments: