Friday, May 11, 2012



TWIGA STARS NA ZIMBABWE KUMEKUCHA KESHO TAIFA


Nyota wa Twiga Stars, Sofia Mwasikili

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kesho inatarajiwa kumenyana na Zimbabwe katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Twiga Stars ambayo ilikuwa katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza imerejea leo (Mei 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam tayari kuikabili Zimbabwe. Ikiwa Mwanza jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi Rock City Queens, lakini mechi hiyo ilivunjika dakika ya 58 kutokana na mvua kubwa. Hadi mechi inavunjika, Twiga Stars ilikuwa ikiongoza kwa mabao 5-0.
Kwa mujibu wa kocha wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa, mechi hiyo itakuwa kipimo kizuri kwao kabla ya kucheza mechi ya mashindano ya Afrika (AWC) dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya kurudiana Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Naye Kocha wa Zimbabwe, Rosemary Mugadza amesema amefurahi kupata mechi hiyo kwa vile anaamini Twiga Stars ni kipimo kizuri kwao kabla ya kucheza mechi yao ya AWC dhidi ya Nigeria.
Twiga Stars na Zimbabwe zilishakutana mara mbili mwaka jana. Mara ya kwanza ilikuwa nusu fainali ya Kombe la COSAFA ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Julai 5 jijini Harare, Zimbabwe ilishinda kwa penalti 4-2.
Mechi ya pili ilikuwa michezo ya All Africa Games (AAG) iliyofanyika Maputo, Msumbiji ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi wa kimataifa Judith Gamba kuanzia saa 10.30 jioni ni sh. 1,000 tu kwa sehemu zote isipokuwa VIP A ambayo ni sh. 10,000 na VIP B ambayo kiingilio chake ni sh. 5,000.

TFF NAO WAMLILIA RACHEL


Marehemu Rachel kulia

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mhariri wa Michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa kilichotokea leo (Mei 11 mwaka huu) katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY, msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani Rachel kwa kipindi chote akiwa mwandishi na baadaye Mhariri alikuwa akifanya kazi nasi, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.
Amesema TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Rachel, kampuni ya New Habari ambayo ndiyo inayomiliki gazeti za Mtanzania na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

POULSEN ATIMULIWA RASMI STARS, MDOGO WAKE AMRITHI


RASMI leo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kummwaga kocha Jan Borge Poulsen katika timu ya taifa, Taifa Stars na kumpa mikoba yake, Kim Poulsen (pichani kushoto) aliyekuwa kocha wa timu za vijana kuanzia leo, Mei 11 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema

AKINA SAMATTA WASHAMBULIWA KHARTOUM, BASI LAO NYANG'ANYNG'AYA


Picha mbalimbali zinazoonyesha uharibu uliofanywa na mashabiki wa Merreikh kwenye gari la akina Samatta










MASHABIKI wa klabu ya Al Merreikh ya Sudan wameufanyia fujo msafara wa klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Khartoum, wakidai na wao walipokewa vibaya na klabu hiyo mjini Lubumbashi wiki mbili zilikzopita.
Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ipo Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora.
Katika vurugu hizo, basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa vioo na athari zaidi ikiwemo hali hali za wachezaji bado hazijajulikana.
Sasa mechi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambayo inatarajiwa kuchukua hatua muda mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta mashindanoni Merreikh na kuifungia hivyo Mazembe kusonga mbele.
Katika mchezo wa kwanza, Samatta, maarufu kama Sama Goal, aliibuka shujaa kwenye Uwanja wa Kibassa Maliba, baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-0.
Kama ilivyokuwa dhidi ya Power Dynamos, safu ya ushambuliaji ya Mazembe inayoundwa na wakali kama Tressor Mputu, Given Singuluma, Kalaba na Samata ilikuwa mwiba mkali.
Mazembe ilipata kona sita wakati wapinzani wao hawakupata hata moja na katika kona hizo ni moja tu iliyozaa matunda kwa Sama Goal kufunga dakika ya 22 kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na Mputu.
Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika Mazembe inayofundishwa na Lamine Ndiaye ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao hilo moja tu.
Nahodha Tressor Mputu aliifungia Mazembe bao la pili dakika ya 70, akipiga shuti zuri nje ya eneo la penalti na mpira kutinga nyavuni upande wa kulia wa lango.
Hakuna kilichobadilika katika dakika 20 za mwisho, licha ya nafasi kadhaa zilizoshindikana kutumiwa vema.
Samatta, Mtanzania aliyetokea Simba SC kujiunga na Mazembe katikati ya msimu uliopita, sasa ana mabao mawili katika Ligi ya Mabingwa ndani ya mechi mbili.
Awali alifunga katika sare ya 1-1 na Power Dymanos ya Zambia, mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora, lakini sikku hiyo aliumia bega na akakosa mechi ya marudiano.



No comments: