Tuesday, May 15, 2012

TAKWIMU YA SIKU: STEWART DOWNING - MECHI 36 BILA GOLI WALA ASSISTS = PAUNDI MILLIONI 20

LOsssssss


Go to Liverpool Team page

19. Stewart Downing

Midfielder Liverpool

GARY NEVILLE KOCHA MPYA MSAIDIZI WA ENGLAND

Mchezaji wa zamani wa England Gary Neville ameteuliwa rasmi na kocha mkuu kuwa mmoja wa makocha wasaidizi wa benchi la ufundi la England aka Three Lions.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, ambaye tangu kustaafu kama mchezaji msimu uliopita, amekuwa akifanya kazi katika kituo cha SkySports kama mchambuzi wa soka, amesaini mkataba wa miaka 4 na chama cha soka cha FA.

Wakati wa enzi za uchezaji wake akiitumikia England alicheza mechi 85, akiiwaikilisha 3 Lions kwenye Euro 96, Euro 2000, Euro 2004, World Cup 98 na World Cup 2006.

"Gary amefanikiwa sana katika mchezo huu akiwa mchezaji wa Manchester United na England," alisema Hodgson. "Ana vyeti vyote vya ukocha vya UEFA na nina uhakika atapata heshima kubwa sana kutoka wachezaji kutokana na uzoefu mkubwa alionao."

Neville mwenyewe aliongea: "Roy aliniita na kuniomba niwe mmoja ya walimu kwenye benchi la ufundi na kufanya nae kazi katika timu ya taifa - jambo ambalo ni heshima kwangu."

BREAKING NEWS: ALLY MAYAI AJIUZULU KUWA MJUMBE WA WA KAMATI YA UTENDAJI YANGA

Legend wa klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans - ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, Ally Mayai Tembele amejiuzulu kuendelea kuwa mmoja wa kiongozi wa wanajangwani hao.


Akiongea na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM, Ally Mayai alisema: "Nimeamua kujiuzulu nafasi ya uongozi wa klabu yangu niipendayo ya Yanga kutokana na jinsi mambo yalivyo ndani ya Yanga. Huu ni uamuzi ambao nimeuchukua bila kushinikizwa na mtu yoyote."


Kwa story zaidi kuhusu suala hili za endelea kutembelea mtandao huu.

PHOTOS: MANCHESTER CITY WATAMBA JIJI LA MANCHESTER - WASHANGILIA UBINGWA MITAANI







QUIZ: FIND THE TURNING POINT OF THIS GRAPH

No comments: