Monday, May 14, 2012

Monday, May 14, 2012

PAMOJA NA KUTOLEWA CAF: RAGE AWAHIDI WACHEZAJI SIMBA MGAO WA MIL.20 ZA VODACOM

Uongozi wa Simba umepanga kuwapa wachezaji wao mgao wa sh 20 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage fedha zitakuwa ni sehemu ya fedha klabu hiyo itakazozipata kutokana na zawadi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

"Wachezaji wamefanya kazi kubwa na kujituma wakati wote wa ligi, hivyo wanahitaji kuzawadiwa ili kuwapa nguvu ya kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao na mashindano ya kimataifa,"alisema Rage.

Timu ya Simba imetwaa ubingwa huo, ambao kwa msimu uliopita ulikuwa unashikiliwa na wapinzani wao wa jadi, Yanga, ambao kwa msimu huu ulioisha mambo yamekwenda kombo kwao na kushika nafasi ya tatu.

Yanga, ambao walitolewa katika hatua za awali za Ligi ya Mabingwa barani Afrika, imekumbwa na mgogoro wa uongozi uliosababisha vurugu klabuni kwao baada ya kupewa kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa wapinzani wao, Simba.

Rage alisema anajivunia mafanikio waliyoyapata msimu huu uliomalizika na kazi nzuri inayofanywa na kocha wao, Mserbia Milovan Cirkovic na ushirikiano uliopo wa viongozi na mashabiki.

SIMBA VS SHANDY: WATANGAZAJI WA TBC NAO WAFANYIWA VITUKO SUDAN

Mtangazaji Jesse John na fundi mitambo Joseph Masanja wa Televisheni ya Taifa (TBC) walikiona cha moto kwenye uwanja wa Ndege wa Khartoum baada ya kulazimishwa kuacha vifaa vyao vya utangazaji kwa madai huenda ni watafiti kuichunguza Sudan.

Pamoja na jitihada za wanahabari hao kujieleza kwa kirefu dhumuni la safari yao kutangaza mechi ya Simba na Al Ahly Shandy, lakini hawakufanikiwa kuingia nchi humo na vifaa vyao.

Kwa mujibu wa John alisema walimpigia simu msemaji wa TFF, Boniface Wambura awasaidie kuwasiliana na viongozi wa shirikisho la soka la Sudan kuomba kuingilia kati ili waachiliwe vifaa vyao, lakini jitihada zao ziligonga mwamba.

"Ni msukosuko, kilichotuleta ni kutangaza mpira, sasa sijui itakuwaje, hii imekuwa ni desturi ya nchi za kiarabu,"alisema John.

Hata hivyo; watangazaji hao walipata visa ubalozi wa Sudan baada ya kupata barua kutoka Tanzania iliyoonyesha kazi ya kutangaza mpira iliyowaleta hapa Sudan.

Sunday, May 13, 2012

RAUL ATUA AL SADD YA QATAR

Raul akipeana mikono na Sheikh wa Qatar, Nawaf bin Nasser al-Thani (kushoto) wakati akikabidhiwa jezi namba 7
Mwanasoka mkongwe wa Hispania, Raul (katikati) akiwasili kwenye sherehe za kutambulishwa kama mchezaji mpya wa Al-Sadd ya Doha, Qatar leo. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 aliyewika katika klabu ya Real Madrid ya kwao, ametua timu hiyo akitokeaSchalke 04 ya Ujerumani, aliyoichezea misimu miwili.

No comments: