Wednesday, April 25, 2012

Wednesday, April 25, 2012

BAADA YA KURUDI LIGI KUU - ANGALIA PRISONS WALIVYOPOKELEWA MBEYA

Mahabiki wa soka mkoa wa Mbeya wakiwa na furaha baada ya kuliona basi wachezaji wa Tanzania Prisons barabarani. Prisons imefanikiwa kupanda daraja baada ya kujaribu kwa takribani misimu kadhaa sasa.

DAR ES SALAAM DERBY COUNTDOWN: YANGA WATUMA SALAMU MSIMBAZI - WAIFUMUA JKT OLJORO 4-1


YANGA, imekumbuka shuka, wakati kumekucha baada ya jana kuichapa JKT Oljoro mabao 4-1, katika mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeweza kufikisha pointi 49 huku ikiendelea kushika nafasi ya tatu, baada ya Azam kufikisha pointi 50 inayoshika nafasi ya pili, wakati Simba inaongoza kwa pointi 59.
Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, imelitema kombe hilo, baada kuboronga mechi mbili huku ikinyang'anywa pointi tatu na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania.
Kamati hiyo, ilichukua uamuzi huo, baada ya Yanga kumchezesha, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi yao dhidi ya Coastal Union, iliyochezwa Machi 31, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Yanga ilimtumia mchezaji huyu ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekudu kutokana na kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo, aliyechezesha mechi yao dhidi ya Azam, Machi 10, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hata hivyo, matarajio ya Yanga kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika mwakani ni finyu, kwani imesaliwa na mechi moja dhidi ya Simba itakayochezwa Mei 5, mwaka huu, Uwanja wa Taifa.
Katika mechi hiyo, Yanga ikishinda itafikisha pointi 52, ambapo Azam itakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 56 iwapo itashinda michezo miwili dhidi ya Toto African na Kagera Sugar, huku ikisubiri hatma ya matokeo ya mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo juzi ulivunjika kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi hiyo, ilivunjika baada ya timu hizo kufunga bao 1-1, lakini mwamuzi wa mchezo huo Rashid Msangi kutoka Dodoma, alivunja pambano hilo, kwa madai Mtibwa waligomea penelti..
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye
Katika mchezo huo wa jana, Yanga iliandika bao dakika ya 36 likifungwa na Hamisi Kiiza, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga la pili dakika 40.
Yanga ikicheza bila Kocha mkuu wake, Kostadin Papic, Kiiza alifunga bao la tatu ikiwa ni dakika moja kabla ya kwenda mapumziko ambapo Pius Kisambale akihitimisha 'sinia' la mabao katika dakika 84.
Bao la kufutia mafunzo la JKT Oljoro lilifungwa na kwa njia ya penelti.

KUTOKA KWA UPUMBAVU WA ZIDANE MPAKA UJINGA WA TERRY JANA: KADI NYEKUNDU ZA KIJINGA ZA MUDA WOTE KWA WACHEZAJI MAARUFU.



BECKHAM LASHES OUT (1998)



Kadi nyekundu maarufu kwa Beckham. Alimpiga teke Diego Simoene katika kombe la dunia la mwaka 1998.


CARRAGHER IN COIN CONTROVERSY (2002)


Jamie Carrragher alitolewa uwanjani kawa kadi nyekundu baada ya umrushia shilingi shabiki wa Arsenal.

BOWYER & DYER EXCHANGE BLOWS (2005)


Kieran Dyer na Lee Bowyer wote wakiwa timu moja waliamua kuubadili uwanja kuwa ulingo baada ya kutwangana wenyewe kwa wenyewe na refa akwazadiwa kadi nyekundu wote wawili.


A ROUND OF APPLAUSE FOR ROONEY (2005)


Baada ya kupewa kadi ya njano kwa kucheza rafu, Wayne Rooney alimpigia makofi usoni mwa refa ambaye nae bila kuchelewa alimpa kadi nyekundu katika ya UCL dhidi ya Villareal.


ROBBEN'S LACK OF CROWD CONTROL (2006)


Arjen Robben alitolewa nje baada ya kufunga goli la ushindi katika dhidi ya Sunderland na kwenda kushabiki na mashabiki ambao walileta tafrani hali iliyopelekea apewe kadi nyekundu.

ROONEY RUBBER-STAMPS ENGLAND EXIT (2006)


Rooney alipewa kadi nyekundu katika mechi ya robo fainali dhidi ya Ureno baada ya kumkanyaga kwa kusudi mchezaji wa Ureno.

ZIDANE LOSES HIS HEAD (2006)


Zidane akiwa on fire aliamua kuendekeza hasira na kumpiga kichwa chizi Materrazi katika mechi ya fainali ya Kombe la dunia 2006 ambapo Itali walitwaa kombe.


SCHOLES' HANDY WORK LANDS HIM IN TROUBLE (2008)


Paul Scholes na ukali wote wa kucheza soka, alipewa kadi nyekundu ya kijinga baada ya kushika mpira kwa makusudi katika mechi dhidi ya Zenit.


SLAP-AN IBRAHIMOVIC (2012)

Zlatan Ibrahimovic alimtandika vibao Aronica katika mechi ya Seria A na kufungiwa mechi 3 za ligi kitu ambacho kinaweza kuwa kwa namna moja ama nyingine kimeathiri sana AC Milan katika mbio za ubingwa.


TERRY'S KNEED-LESS RED CARD (2012)


John Terry jana aliigahrimusana timu yake ya Chelsea baada ya kumpiga na goti Alexis Sanchez kwenye makalio.

WAARABU WA SIMBA - AL ALHLY SHANDY KUDONDOKA BONGO KESHO - KUWAONA DHIDI YA SIMBA NI 5000 - 3000

SIMBA SPORTS CLUB
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|
WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
25/04/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU waandishi.
Kama mnavyofahamu, Jumapili ya Aprili 29 mwaka huu, timu ya soka ya Simba inakutana na klabu ya Al Ahly Shandy kutoka Sudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ni timu pekee kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote ya kimataifa inayosimamiwa na CAF.
Kubwa zaidi, ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa na hivyo wanabeba bendera ya taifa kokote kule waliko.
Maandalizi yote kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.
Wapinzani wetu, Al Ahly wanatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines.
Waamuzi na Kamishina wa mchezo wamepangwa kuwasili Ijumaa (keshokutwa) wakitokea nchini Swaziland na Rwanda.
VIINGILIO
Kutokana na ukweli kwamba mechi hiyo itakuwa ya kimataifa, Simba imepanga viingilio ambavyo kila mwananchi ataweza kuvimudu. Viingilio vitakuwa kama ifuatavyo.
Viti vya bluu na kijani itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP A 30,000.
Tiketi zitauzwa katika maeneo yafuatayo, Big Bon, Benjamin Mkapa, Stears Mjini, Mbagala Dar Live, OilCom Buguruni, Tandika Mwembeyanga, Ubungo Oilcom, Mwenge Bus Stand, BP Mwananyamala na Gapco Ukonga.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa asubuhi katika maeneo yaliyotajwa.
Klabu imepokea maombi mengi kutoka kwa wanachama na wapenzi wake kutoka mikoani na ingeomba kwamba wale wanaotaka kuja kutazama mechi hii kwa makundi kutoka mikoani, wawasiliane mapema na uongozi ili wanunuliwe tiketi zao mapema.
Simba SC imechapa tiketi za kutosha na ingeomba wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo.
Wana Simba wote wanaombwa kuja uwanjani wakiwa wamevalia mavazi yao ya rangi Nyekundu na Nyeupe ili uwanja mzima upendeze kwa rangi hizo.
Tunatoa wito kwa vyombo vya habari kuisaidia Simba na Tanzania kwa kuelekeza nguvu zao katika uandishi wa taarifa ambazo zitaisaidia timu yetu kusonga mbele na si kuondoa morali au kusababisha watu wasiende uwanjani.
Shukrani.
Uongozi wa Simba SC unatoa shukrani, kwa namna ya kipekee kabisa, kwa serikali kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa kujiandaa na mechi hii muhimu.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba SC

KWANINI KILA SIKU NI AZAM TU: MECHI YAO YA 3 REFA AWA CHANZO CHA MATATIZO MCHEZONI.




Kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi miwili, juzi refa aliyechezesha mechi ya Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, alikuwa chanzo cha matatizo mchezoni.
Mtibwa waligomea mechi na kuondoka uwanjani wakiwa wamefungana 1-1 na Azam FC, Uwanja wa Azam, Chamazi.
Msimu uliopita Mtibwa Sugar walifungwa nyumbani na Azam mabao manne, hawakuleta tatizo, lakini juzi wakiwa wapo 1-1 wakaamua kugoma.
Waligoma baada ya kuchoshwa na maamuzi mabovu ya refa, ikiwemo kuwapa penalti ambayo si halali wenyeji.
Marefa wakisindikizwa na polisi katika mechi dhidi ya Yanga na Azam
Hii ni mara ya tatu ndani ya miezi miwili, marefa wanaochezesha mechi za Azam wanakuwa sababu ya kuvurugika kwa mchezo.
Wiki mbili zilizopita tu, refa aliyechezesha mechi kati ya Azam FC na wenyeji Polisi Dodoma, Uwanja wa Jamhuri alipigwa na mashabiki baada ya mechi.
Azam ilishinda 1-0, beo pekee la beki wake wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Aggrey Morris Ambroce dakika ya 83 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Polisi Dodoma.
Katika mchezo huo, Polisi Dodoma, ilipata pigo baada ya beki wake, Bakari Omari kutolewa nje kwa kadi nyekundu, dakika ya 57 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Refa wa mchezo huo alipigwa na mashabiki kwa madai ya kuwapendelea Azam, baada ya mpambano kukamilika, lakini askari walifanikiwa kumuokoa asipokee kipondo zaidi.
Awali, mwezi uliopita, refa aliyechezesha mechi kati ya Yanga na Azam, Israel Nkongo alipigwa na Stefano Mwasyika na angeweza kupigwa pia na mashabiki wa Yanga.
Kwa nini apigwe? Kisa kutuhumiwa kuipendelea Azam. Mechi zinazochezwa kwenye Uwanja wao, timu nyingi zimekuwa zikilalamika Azam inabebwa.
Kwa muda mrefu wapenzi wa soka Tanzania wamekuwa wakilalamikia desturi ya klabu kongwe nchini Simba na Yanga kutamba nyumbani, kudaiwa kushinda kwa kununua mechi.
Hii inasababisha timu zetu zinakuwa dhaifu kwenye michuano mikubwa na ndiyo maana zinashindwa japo kucheza hatua ya makundi tu ya michuano ya Afrika.
Watu wanataka timu ishinde kwa uwezo, ili idhihirishe ubora ambao utakwenda kuifanya ishiriki vyema michuano ya Afrika.
Kwa sababu hiyo, ujio wa Azam FC timu inayomilikiwa na Milionea Said Salim Bakhresa ulipokewa kwa furaha na wadau wa soka nchini, wakijua amepatikana mkombozi wa kweli.
Azam imewekeza fedha nyingi kuanzia kwenye usajili, ajira za makocha, Uwanja wake kule Chamazi- na kwa ujumla ni timu ambayo ukiangalia inapoelekea unajenga matumaini.
Azam haina wanachama wa kuleta mizengwe ya kuvuruga timu, wanaweza kujivuruga wao kwa wao tu.
Mchezaji wa Azam hachezi kwa presha ya kutukanwa na mashabiki akikosea kama mchezaji wa Yanga au Simba. Azam imesajili wachezaji nyota kuanzia ndani na nje ya nchi.
Azam inaongoza kutumia fedha nyingi na kusajili wachezaji bora nchini. Hivyo timu hii inastahili kuwa bingwa wa nchi kulingana na jinsi ilivyowekeza.
Lakini wasiwasi ni kwamba, mechi zao zinatiliwa shaka sasa nao kama wanatumia mbinu chafu ikiwemo kuhonga marefa ili kushinda.
Kama kweli watakuwa wanafanya hivyo, ina maana watakuwa wanaiga Simba na Yanga, ambazo kimsingi zinanyooshewa kidole kwa kudumaza maendeleo ya soka ya nchi hii.
Kama Azam wanaiga Simba na Yanga kununua mechi, wanaweza wakafanikiwa kuwa mabingwa, lakini swali la kujiuliza soka ya Tanzania itakuwa kweli imepata mkombozi?
Napata shaka sana juu ya mustakabali wa soka ya nchi hii, ikiwa Azam nayo inakuja kwa staili hii- dhahiri bado tuna kazi ngumu na safari ndefu kufikia japo karibu na mafanikio.
Kwa sababu mchezaji akishajua kwamba kuna unafuu katika mchezo kutokana na mabosi wao kuhonga, hawezi kujituma tena kwa sababu anajua ushindi upo tu.
Mwaka 2007, baada ya Yanga kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Esperance ya Tunisia, aliyekuwa kipa wa timu hiyo, Ivo Mapunda aliwashauri viongozi wa klabu yake wakati huo, wawe wanafanya mipango na marefa kurahisisisha mechi.
Tayari mchezaji kujenga dhana hiyo- inamaanisha amefikia mwisho wa uwezo wake, wakati suluhisho ni kufanyia kazi mapungufu ili wakati mwingine ufanye vizuri.
Mwaka juzi, Simba ilifungwa 5-0 na Haras El Hodood nchini Misri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, mwaka jana ilifungwa 3-0 na Wydad Cassablanca, mara zote ikitolewa katika michuano ya Afrika.
Mwaka huu, imefungwa 3-1 ikitoka kushinda 2-0 nyumbani na ES Setif moja ya timu tishio tu Afrika na kuingia hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho.
Hii nini maana yake? Simba imefanyia kazi mapungufu kutoka kufungwa 5-0, 3-0 na 3-1 sambamba na kusonga mbele.
Lakini desturi ya kutaka kurahisisisha kazi kwa kununua mechi- maana yake hatuwezi kufanyia kazi mapungufu.
Kweli wapenzi wa soka Tanzania wanaitegemea Azam iijengee heshima nchi hii katika michuano ya Afrika, lakini kwa staili ambayo wanataka kwenda nayo. Hakuna hakika kama watafanikiwa.
Yapo maneno tayari yanasemwa semwa kuhusu Azam na harakati zao za ubingwa na mbinu wanazodaiwa kutumia hadi watu wanaodaiwa kutumiwa kutoka kwenye mamlaka husika- japo kwa sasa tunayachukuliwa kama maneno ya mtaani tu, lakini ipo haja ya kuiangalia Azam kwa jicho la tatu.
Haina maana Yanga kukosekana michuano ya Afrika mwakani, wakati ilipigana kwa uwezo wake na kuzidiwa na timu ambayo ushindi wake ulitokana na mbeleko za marefa.
Namna hii hata mtu huwezi kustaajabu kwa nini John Bocco mabao yake anafunga Azam tu na timu ya taifa anabaki yeye na kipa mara kibao anashindwa. Akizomewa eti anasusa.
Watu hawataki kujadili ukweli wa kiini cha tatizo, kwa sababu tayari kuna kosa lilitendeka- lakini hawajui kwamba hata kosa lina sababu.
Jasiri yoyote hakubali kudhulumiwa haki yake bana- tusidanganyane na wala watu wasitake kujiona wao miungu watu katika dunia hii- misingi ya haki ni ile ile.
Kila jina zuri lina jina mbadala la uasi- watu wakikupenda kwa ujasiri wako wa kutopenda kuonewa kiasi cha kuwa tayari kupambana na yeyote kutetea haki, watakuita jasiri, shujaa, shupavu.
Lakini kwa sababu hizo hizo, wakiwa hawakupendi watakuita mkorofi- mgomvi, huelewani na watu- hiyo ndio dunia yetu ya leo- dunia tofauti na ile waliyoishi akina Mtemi Mirambo, Chifu Mkwawa na Adolph Hitler.
Mtibwa walikuwa wastaarabu wakaondoka uwanjani- hawajui mbali na kupoteza pointi tatu, watatozwa faini na sijui kanuni zinasemaje zaidi, ili kuna hatari ya kufungiwa pia kucheza ligi.
Wachezaji wa Yanga waliona bora kumtandika Nkongo- hawakujua mbele yake kuna kufungiwa kucheza na kuigharimu zaidi klabu yao.
Lakini chanzo cha yote haya ni nini? Azam hao. Wanafanya nini, sijui na sina ushahidi kama wanahonga marefa na siwezi kusema wanahonga marefa, ila naweza kujiuliza kwa nini wawe wao tu? Mara moja bahati mbaya- lakini sasa mara ya tatu jamani, timu hiyo hiyo moja! Hapana bwana!

Source: www.bongostaz.blogspot.com

CHEKA AJIFUA KUMKABILI MAUGO JUMAMOSI HII


Kocha wa mchezo wa Masumbwi Abdalah Ilamba 'Komandoo' akimfanyisha mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo bondia Francis Cheka Dar es salaam jana Chaka anajiandaa na mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atakuwa bingwa wa Mkanda wa I.B.F na atanyakua Zawadi ya gari.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, April 24, 2012

WANAUME WA 10 WA CHELSEA WAMLIZA MESSI - WAIVUA UBINGWA BARCELONA


Barcelona 2-2 Chelsea -24.04.2012-Geniş Özeti HD... by canliveiddaa

Exclusive interview: JOSEPH OWINO - ' SASA NIMEPONA '

SUAREZ DHIDI YA AKINA ROONEY - BRAZIL WAPANGWA KUNDI MOJA NA MISRI - OLYMPIC 2012



Out of the hat: Brazil legend Ronaldo was on hand to help with the draw
Brazil legend Ronaldo akitangaza makundi ya michezo ya Olympic itakayofanyika nchini Uingereza .

GROUP A
Great Britain
Senegal
UAE
Uruguay

Fixtures: July 26, Manchester, UAE v Uruguay, Great Britain v Senegal; July 29, London, Senegal v Uruguay, Great Britain v UAE; August 1, Cardiff, Great Britain v Senegal; Coventry, Senegal v UAE

GROUP B

Mexico
North Korea
Gabon
Switzerland

Fixtures: July 26, Newcastle, Mexico v N Korea, Gabon v Swiss; July 29, Coventry, Mexico v Gabon, N Korea, Switss; August 1, Cardiff, Mexico v Swiss; London, N Korea v Gabon

GROUP C

Brazil
Egypt
Belarus
New Zealand

Fixtures: July 26, Coventry, Belarus v New Zealand; Cardiff, Brazil v Egypt; July 29, Manchester, Brazil v Belarus, Egypt v New Zealand; August 1, Newcastle, Brazil v New Zealand; Glasgow, Egypt v Belarus

GROUP D

Spain
Japan
Honduras
Morocco

Fixtures: July 26, Glasgow, Spain v Japan, Honduras v Morocco; July 29, Newcastle, Spain v Honduras, Japan v Morocco; August 1, Coventry, Japan v Honduras; Manchester, Spain v Morocco

BUNDI AZIDI KUTAWALA ANGA LA JANGWANI: KIONGOZI MWINGINE

EXCLUSIVE INTERVIEW: MSIKILIZE RUUD GULLIT

FIRST DIVISION LEAGUE FINALS 2011 - 2012


NO TEAMS P W D L GF GA GD PTS YLW RED TOTAL
1 Polisi Moro FC 8 6 2 0 16 5 11 20 12 0 12
2 Mgambo Shooting 8 4 3 1 12 6 6 15 15 1 16
3 Tanzania Prisons 8 4 2 2 10 6 4 14 12 0 12
4 Polisi Dar FC 8 3 4 1 11 4 7 13 11 1 12
5 Mbeya City FC 8 3 2 3 10 8 2 11 8 1 9
6 Rhino Rangers FC 8 2 2 4 4 8 -4 8 9 1 10
7 Mlale JKT 8 2 2 4 8 15 -7 8 7 1 8
8 Polisi Tabora FC 8 1 3 4 7 14 -7 6 8 0 8
9 Transit Camp 8 0 2 6 3 15 -12 2 7 0 7
TOTAL 36 13 11 13 81 81 0 97 89 5 94
AS FOR: 23.04.2012
Average of Goal per game 2.3
Average of Yellow Cards per game 2.5
Average of Red Cards per game 0.1
Average of Total Cards per game 2.6

No comments: