Sunday, April 8, 2012


Ubwa apewa mikoba ya Mwasika

ABOU Ubwa anaandaliwa kucheza nafasi ya beki wa kushoto ya Yanga katika mechi dhidi ya Toto Africa itakayopigwa Aprili 15

Uamuzi huo unatokana na Oscar Joshua na Stephano Mwasika
kutumikia adhabu. Mwasika amefungiwa mechi tano na Oscar anatumikia kadi tatu za njano.

Ubwa amekuwa akikalia benchi kwa sababu ya ushindani wa namba ambayo ilikuwa ikishikwa na Mwasika.
Mbali na hao, Yanga itamkosa pia Juma Seif 'Kijiko' ambaye naye ana kadi tatu za njano.

No comments: