Baadhi ya wageni waalikwa na wanachama wa Kituo cha Ushauri na Msaada wa Kisheria Mtwara PARALEAGEL wakiwa katika ufunguzi wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani. |
Juma Mohamed, Mtwara
Ikiwa Jamii
inaelekea kuadhimisha siku ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia Desemba 10 mwaka
huu, huko mkoani Mtwara matukio ya aina hiyo yanawakumba wanaume lakini
wanashindwa kuyaripoti kutokana na sababu mbalimbali.
Wakizungumza
katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na kituo cha ushauri msaada
wa kisheria PARALIGO mkoani humo, baadhi ya wanaume walitoa ushuhuda wa matukio
hayo licha ya jamii kuamini kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo ni wanawake na
watoto.
“Kwa mfano
kuna jirani yetu mmoja hivi akirudi nyumbani mkeo anamfungia ndani anampiga
hata kama akitimiza mahitaji yote..alafu tena anamsachi mfukoni anamchukulia
chochote ambacho anacho asubuhi Yule mwanaume anadharau anaenda kufanya kazi
zake kama kaiwaida..” alisema Shaibu Salum mkazi wa Mtwara.
Naye
mwenyekiti wa dawati la jinsia mkoa wa Mtwara Bahati Sembela, anaeleza
kukithiri kwa malalamiko juu ya vitendo hivyo huku akidai kuwa waathirika
wakubwa ni wanawake na watoto
Maadhimisho
hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yamezinduliwa leo mkoani Mtwara
ambapo yanafikia mwaka wa 9 sasa toka kuanza kuadhimishwa kwake mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment