Na Evelyn Mkokoi, Geita
Mgodi maarufu wa kuchimba dhahabu mjini Geita wa GGM
umekumbana na adhabu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC
katika Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Mkoani Geita kwa kosa la
kukosa vyoo vya wafanyakazi zaidi ya mia tatu (300) katika eneo la chini ya
ardhi underground la uchimbaji wa
madini ya dhahabu.
Hali hiyo imeipelekea NEMC kuutoza mgodi huo faini ya shilingi
milioni 10, zinazotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne.
Katika ziara hiyo iliyomlazimu Naibu Waziri Mpina kuvaa vifaa
maluum ili kuweza kuingia katika eneo la
chini ya ardhi lenye mwamba mkubwa wa mgodi huo, akiambatana na baadhi ya
maafisa aliongozana nao katika ziara yake, Naibu Waziri alijionea namna ambavyo
eneo lenye idadi kuwa ya wafanyakazi kukosa
huduma hiyo muhimu ya choo
inayowapelekea kujisaidi vichakani na kuharibu mazingira.
|
Aidha Naibu Waziri Mpina Pia aliweza kujionea uharibifu
mwingine unaofanywa na mgodi huo wa utiririshwaji wa Maji ya mvua
yaliyochanganyikana na madawa hatarishi kwa mazingira na viumbe hai kwenda kwenye makazi ya wananchi.
Kufuatia hali hiyo, Naibu waziri Mpina alielekeza uongozi wa
mgodi huo kujenga miundombinu rafiki kwa mazingira yatakayopelekea maji hayo
kwenda katika mkondo sahihi..
|
Akiongea kwa Niaba ya GGM makamu wa Rais wa Mgodi
huo Bw. Simon Mushy, alisema kuwa wapo kwenye mchakato wa kujenga miundombinu
kwa kushiriana na Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kwa upande wa mmoja wa
wakazi wa kijiji cha Katoma Bi. Magori James Katoka alisema kuwa vumbi na maji ya mvua
vinavyotoka kwenye mgodi huo vimekuwa ni kero na changamoto ya muda mrefu
katikma kijiji hicho.
Pamoja na malalamiko mengi ya wakazi wa Katoma Geita kuhusu
uharibifu wa mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi huo pia umefanya
shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambza maji safi a salama
katika mji wa Geita ukishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mkoa huo.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Kaika Mkoa wa geita ni muendelezo
wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira, viwanda na migodi nchini.
No comments:
Post a Comment