Na
Mwandishi Wetu Juma News
WASHINDI wawili, Exaudi Mgeni wa Iringa na Joel Mwakagali wa Mbeya, waliojinyakulia jumla ya kitita cha Sh milioni 82, wamekabidhi wa fedha zao jana katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Bosi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Abbas Tarimba.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano ya hundi yenye thamani ya fedha hizo, Tarimba aliipongeza m-Bet kwa kuendesha mchezo huo kwa ufanisi, lakini pia washindi hao kwa kuibuka kidedea.
Alisema bodi yake inafarijika kuona washindi hao wakiliingizia pato Taifa kupitia kodi watakayolipa kwa kushinda fedha hizo ambazo ni kama Sh milioni saba hivi, huku akiwataka kuhakikisha wanazitumia ipasavyo fedha hizo kuboresha maisha yao.
“Michezo ya –ku-bet’ tumeweza kuilea ili kutoa nafasi kwa wanamichezo kushiriki michezo hii ya kubahatisha ambayo ni neema kwa taifa na si janga kama baadhi ya watu wanavyodhani,” alisema Tarimba.
Mkurugenzi Mku wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba akizungumza kwenye hafla ya kuzawadia washindi wa M-bet jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2016. |
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kaba, alisema kuwa Mgeni na Mwakagali, walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 12 za ligi za Ulaya kwa Super 12.
“Tunafarijika kuwakabidhi kitita chao cha Sh milioni 82 Joel na Exaudi kama washindi wa m-Bet ambao kila mmoja atapata Sh milioni 41 kabla ya makato ya kodi,” alisema Kaba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Super 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote kama Mgeni na Mwakagali, unaondoka na kikapu cha siku.
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Super 1x2 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-bet,” alisema Kaba.
No comments:
Post a Comment