Na Juma Mohamed.
WAMILIKI wa
mitandao ya mawasiliano nchini wametakiwa kutoa taarifa haraka juu ya makosa ya
uharifu wa mitandaoni pindi yanapojitokeza, ili kuwarahisishia watu wa vyombo
vya usalama kuweza kuchukua hatua za haraka kwa wahusika.
Wito huo ulitolewa
jana mkoani hapa na mkuu wa upelelezi Polisi wilaya ya Masasi, SP Nathaniel
Kyando, wakati wa Semina ya mahakimu, waendesha mashitaka na wapelelezi kuhusu
elimu ya sheria ya makosa ya mtandao na sheria ya miamala ya kielektroniki ya
mwaka 2015.
Alisema, sheria
hiyo ambayo imeanza kufanya kazi Septemba 1 mwaka huu, ilitakiwa kutolewa
mapema kwasababu yapo makosa mengine ambayo tayari yameshatendeka ambayo
yalipaswa kudhitiwa kwa watendaji wake.
“Kumekuwa na
tatizo kwa wamiliki wa vyombo vya mitandao kama watu wa simu, taarifa hua
hawazitoi kwa muda muwafaka kiasi kwamba upatikanaji wa waalifu wa kimtandao
mara nyingine unakuwa ni wa shida sana..lakini pamoja na uwepo wa sheria hii,
ni muhimu sasa wamiliki wa vyombo vya mitandao wakaona umuhimu wa kutoa taarifa
kwa wakati..” alisema.
Kwa upande
wake, mkuu wa kitengo cha sheria kutoka wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Veronica Sudayi, akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara
hiyo, alisema jamii inatakiwa kufahamu kwamba sheria hiyo haina vitu vipya
isipokuwa ni mabadiliko ya kimfumo ambayo umeyaingiza makosa hayo katika mfumo
wa kielektroniki.
“Zamani
kabla ya sheria hii ilikuwa unashindwa kumtia hatiani mtu aliyefanya uhalifu
kwa kutumia mfumo kwasababu kile kitendo cha kushika anaweza asikifanye, lakini
kwa sasa sheria hii itamtia hatiani kwasababu hata ukionekana ukioneka fedha
kwa kuhamisha kutoka akaunti moja kwenda nyingine na ikathibitika basi utatiwa
hatiani..” alisema.
Alisema,
mwanzoni jamii ilikuwa na dhana potofu juu ya sheria hiyo kwa kudhani kwamba
watu wengi watukuwa wanaingia jela lakini kwa kiasi fulani sasa wanaanza
kuelewa na kutii yale maadili yanatopaswa kufuatwa kwa watumiaji wa mitanado.
Aidha,
alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wahusika ambao ni Mahakimu,
wapelelezi na waendesha mashitaka wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma na majaji
wote ili wanapotekeleza majukumu yao juu ya sheria hiyo haki itendeke.
Naye, mwanasheria
kutoka wizara hiyo, Anna Kalamo, alisema miongoni mwa mada ambazo wanapatiwa
wahusika ni pamoja na sheria mbili ambazo zimepitishwa na serikali za miamala
kielektroniki na sheria ya makosa ya mitandao zote za mwaka 2015 ambazo zimetungwa
kwa lengo la kuleta ulinzi na matumizi salama ya mitandao hapa nchini.
Anna Kalomo |
Alisema kuna
athari nyingi ambazo zinatokana na makosa ya mitandaoni ambayo miongoni mwake
ni kuibiwa, watu kujiua kutokana na kudhalilishwa, kuvunjika kwa ndoa za watu
pamoja na hasara mbalimbali katika taasisi za kifedha kama Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) ambayo ilitangaza hasara ya karibu bilioni 54.
No comments:
Post a Comment