Mshindi wa Fiesta Supa Nyota mkoani Mtwara, Willy Dismiler akiwa na Jaji wa shindano hilo Nickson George, baada ya kutangazwa mshindi. |
Baadhi ya washiriki wa shindano la kusaka vipaji la Fiesta Supa Nyota, lililofanyika mjini Mtwara katika ukumbi wa bwalo la polisi wa Makonde beach. Mshindi katika shindano hilo ni Willy Dismiler. |
Juma Mohamed, Mtwara
Fiesta Supa
Nyota imemuibua kijana Willy Dasmailer kutoka mkoani Mtwara ambaye atapanda
katika jukwaa la Fiesta kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa mkoa huo katika
shoo itakayofanyika kesho katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kijana huyo
ambaye alifanikiwa kupenya katika mchujo uliowajumuisha jumla ya vijana 96
wenye vipaji waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, aliwashukuru waandaji wa Fiesta
na mashabiki zake pamoja na kuahidi kufanya vyema katika hatua zijazo.
“Nashukuru
sana na nawaahidi tu mashabiki wangu kama Dasmiler nitazidi kuwa nao, sio kwa
hapa nyumbani tu hata nikiwa wapi nitazidi kuwakumbuka..mchango wenu pia
umefanikisha mimi kufika hapa, nawashukuru sana..” alisema.
Maarifa NIC ni
mshindi wa pili wa mchuano huo mkali na kuelezea mchakato ulivyoenda pamoja na
matarajio yake katika Fiesta ijayo “nashukuru kwa nafasi hii ya namba mbili
nawahidi kwamba sitokata tamaa” alisema.
Washiriki wa Fiesta Supa Nyota Mtwara walioingia Tano Bora wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi Willy Dismiler pamoja na Jaji wa shindano hilo, Nickson George. |
Jaji mkuu katika shindano hilo Nickson George alizungumzia
zoezi zima lilivyoenda pamoja na ugumu alioupata katika kumtafuta Supa Nyota
huyo, ambapo alidai kuwa aina uimbaji kufanana ni moja ya changamoto ambayo pia
alikumbana nayo katika maeneo mengi ya kusaka vipaji hivyo.
Mshindi huyo
wa Supa Nyota atapanda katika jukwaa moja na wasanii wengine wakubwa hapa
nchini katika tamasha la Fiesta hapo kesho, pamoja na kupafom katika fainali ya
tamasha hilo itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment