Kikosi cha Ndanda FC msimu wa 2015/2016 |
Na Juma Mohamed, Mtwara
TIMU ya soka
ya Ndanda FC ya mkoani hapa imepangwa kuanza ugenini na wekundu wa Msimbazi
Simba Sports Club, katika michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu
huu wa 2016/2017.
Kwa mujibu
wa ratiba ya ligi hiyo iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), inaonesha ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka
huu, huku ‘Wanakuchele’ Ndanda FC wakianzia ugenini dhidi ya Simba na Mtibwa
Sugar kabla ya kurejea Nangwanda kuvaana na Yanga.
Akizungumza na
Juma News, afisa habari wa Ndanda, Idrissa Bandari amesema wao wameipokea vyema
ratiba hiyo na kwamba kwa sasa wanakiandaa vyema kikosi chao ili kiwe imara kwa
ajili ya kuimili mikimikiki ya ligi hiyo.
Kikosi cha Simba SC msimu wa 2015/2016 |
“Vyovyote
ingekuja, tungechukulia uzito kama ratiba zingine kama ambavyo zinakuja kwetu
kuwa na uzito mkubwa, kwahiyo tunaimani kwa ratiba hii pia ni ngumu lakini
tunakwenda nae hivyohivyo kama ilivyo..sio mechi rahisi ni mechi ngumu
tunazoanza nazo lakini hakuna mechi yeyote kwenye ligi inayokuwa ya kwanza,
katikati au yamwisho ikawa rahisi..” alisema Bandari.
Katika hatua
nyingine, Bandari alisema wamekuwa wakizisikia taarifa za kocha wao Malale
Hamsini kujiunga na klabu ya JKT Ruvu ya Pwani na kwamba leo jioni uongozi
unakaa kikao ambacho kitajadili juu ya suala hilo, huku Malale mwenyewe akidai
kuwa mustakabali wake utatokana na maamuzi ya klabu ya JKU ya Zanzibar ambayo
ndio mwajiri wake.
1 comment:
Duh kazi kazi....
Post a Comment