Wanafunzi wa shule za msingi Maendeleo na Rahaleo wakisubiri zamu ya kuingia Msalani. |
Vyoo ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Maendeleo..kwasasa vimefungwa kutokana na kuwa vibovu. |
Choo kinachotumiwa na walimu wa shule mbili za msingi, Maendeleo na Rahaleo za manispaa ya Mtwara Mikindani. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Wakati mkoa
wa Mtwara ukisimama kifua mbele kutokana na kufanikiwa kumaliza tatizo la
madawati kwa shule za msingi na sekondari kwa Zaidi ya asilimia miamoja, bado
unakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya majengo katika shule
mbalimbali.
Shule ya
msingi Maendeleo iliyopo manispaa ya Mtwara Mikindani, ni miongoni mwa shule
zinazokabiliwa na changamoto hiyo kutokana na wanafunzi wake kulazimika kupanga
foleni kusubiri zamu ya kuingia chooni kujisaidia hali ambayo inawafanya
wapitwe na sehemu ya vipindi vya darasani, kwasababu shule hiyo haina vyoo na
kujikuta wanadoea vyoo vya shule ya Rahaleo.
“Tunapata
shida ya usafi kwasababu, kama sisi tuliokua huku kule choo kikichafuka kidogo
tunalaumiwa sisi kuwa ndio tuliochafua kwasababu kule chooni kunatupiwa makopo
kwamfano watoto wa Awali wakitupa makopo tunachukuliwa darasa la Saba kwenda
kudeki, kwahiyo huku ndani tunakosa vipindi na mwalimu anakuwa ameshafundisha..”
alisema Mashaka Fadhili.
Thabiti Hussein-mwanafunzi wa shule ya msingi Maendeleo, manispaa ya Mtwara Mikindani |
Thabiti
Hussein, mwanafunzi wa Maendeleo aliiomba serikali kufanya jitihada za
kuwajengea vyoo ili waondokane na adha wanayoipata kutokana na kutumia muda wa
masomo kufanya usafi vyooni.
Changamoto
hiyo haijaishia kwa wanafunzi pekee, bali hata kwa walimu ambao ni Zaidi ya
Arobaini kwa shule zote mbili za Rahaleo na Maendeleo, wanalazimika kutumia
matundu mawili ya vyoo na kujikuta wanapanga foleni kusubiri zamu.
Choo cha shule ya msingi Maendeleo |
“Sisi walimu
choo chetu tunatumia matundu mawili wanaume na wanawake, kwahiyo choo kipo
lakini tuna ‘share’ na Rahaleo hichohicho kimoja..kwahiyo hua tunapanga foleni
kwakweli hata vyoo vya walimu havitoshelezi kwahiyo nilikuwa naomba serikali
inaposikia jambo hili itupie macho kwa ujumla kwamba sisi shule ya msingi
Maendeleo tunachangamoto nyingi..” alisema Fabiola Haule, mwalimu mkuu wa shule
ya Maendeleo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maendeleo, manispaa ya Mtwara Mikindani-Fabiola Haule. |
Naibu Meya
wa manispaa hiyo, Erick Mkapa ambaye ni diwani wa kata ya Rahaleo, alikiri
kuwapo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa anafanya juhudi za kuwashirikisha
wadau mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha wanatatua tatizo hilo.
Choo cha
shule ya msingi Maendeleo ambayo ilianzishwa mwaka 2007 ilipogawanywa kutoka
shule ya Rahaleo, kimefungwa kwa takribani miaka mine sasa kutokana na
kutokidhi kwa matumizi ya wanafunzi.
'Toka nije mimi' |
No comments:
Post a Comment