Ushindi rahaaaaaa |
Twapongezana baada ya ushindi |
Tuzo zikisubiri washindi katika maonyesho ya Young Scientists Tanzania mkoa wa Mtwara. |
Picha ya pamoja washindi wa nafasi mbalimbali katika maonyesho ya Young Scientists Tanzania mkoa wa Mtwara na waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prf. Joyce Ndalichako |
Mshindi mwenza katika nafasi ya kwanza katika maonyesho ya Young Scientists Tanzania mkoa wa Mtwara, Jacqueline Munisi kutoka shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi. (Mtwara Technical) |
Mshindi mwenza katika nafasi ya pili kwenye maonyesho ya Young Scientists Tanzania mkoa wa Mtwara, Diana Sosoka kutoka shule ya sekondari ya Wasichana Mtwara. (Mtwara Girls) |
Juma Mohamed, Mtwara
Serikali
imewataka wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini kujikita
zaidi katika kusoma masomo ya Sayansi ili kuliongezea Taifa wataalamu hasa
katika kuunga mkono sera ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John
Magufuli inayohitaji kuwa na Tanzania yenye viwanda.
Akizungumza
katika kilele cha maonyesho ya Teknolojia na Wanasayansi Vijana kutoka shule
mbalimbali za sekondari mkoani Mtwara, waziri wa elimu, sayansi na teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako, amesema wizara yake itaongeza fursa nyingi katika
masuala ya sayansi na teknolojia kwa kutambua mahitaji yaliyopo.
Mkurugenzi
na mwanzilishi mwenza wa maonyesho hayo Dokta Gosbert Kamugisha, amesema vijana
hao ambao walitumia muda wa miezi sita kuandaa maonyesho hayo wako tayari
kufanya masuala ya sayansi ta teknolojia kwa masilahi ya Taifa, huku washindi
wa kwanza na wapili katika maonyesho hayo kutoka shule za Mtwara Ufundi na
Mtwara Wasichana wakielezea furaha zao baada ya kutangazwa washindi.
Tazama Video hapa chini >>>
Tazama Video hapa chini >>>
Washindi
waliopatikana kupitia maonyesho hayo ambayo yalihusisha shule Arobaini mkoani
Mtwara watauwakilisha mkoa huo katika maonyesho yakitaifa yatakayofanyika mwezi
huu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment