Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani- Nairobi, Daniel Ogembo (PICHA: MTANDAO) |
Na
Mack Kemoli, Nairobi.
Mahakama
Nairobi imeamuru wabunge wanane waliokamatwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi
wanashikiliwa na jeshi la polisi mpaka Ijumaa juni 17 mwaka huu, wakati kesi
yao itasikilizwa tena.
Hakimu
mkuu wa mahakama ya Milimani- Nairobi, Daniel Ogembo alisema kwamba wabunge hao
wabaki korokoroni huku idara ya upepelezi ikikusanya ushahidi wa kutosha
wa kuwashtaki.
Akikubaliana
na ombi la mwendesha mashtaka, Sajenti Gilbert Kitalia , hakimu huyo aliamua
washilikiwe katika vituo vya polisi vya Kilimani, Gigiri, Pangani, Kileleshwa,
Muthangari na Muthaiga hadi ijumaa watakapofikishwa mahakamani.
Wabunge
hao ,Moses Kuria (Gatundu South) , Ferdinand Waititu (Kabete), Kimani
Ngunjiri (Bahati) wote wa mrengo wa Jubilee unaoongozwa na wenzao, Johnstone
Muthama (Machakos), Junet Mohamed (Suna East), Aisha Jumwa (Kilifi), Florence
Mutua (Busia) na Timothy Bosire (Kitutu Masaba) wa mrengo wa cord( upinzani),
walikuwa wamekamatwa awali na kupelekwa kwenye idara ya upelelezi ambapo mkuu
wa police nchini Kenya Boinnet aliamuru wasiachiliwe.
Kisa
cha wabunge hao kukamatwa kilianza Jumapili ambapo vyombo vya habari vilimnukuu
mbunge wa Gatundu South, Moses Kuria - anapotoka rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
akisema kwamba Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga anasumbua na kwamba anastahili
apigwe risasi ili nchi iendelee.
Matamshi
hayo hayakuchukuliwa vyema na wabunge wa upinzani wakiongozwa na mbunge Junnet
Mohammed aliyesema kwamba hawatishwi na serikali na kwamba hao (upinzani)
wana uwezo wa kutisha hata kuua.
Wabunge
zaidi waliweza kutoa vitisho kwa wenzao wa aidha upande wa serikali au
upinzani.
Kisheria,
endapo wabunge hao watapatikana na hatia, huenda wakafungwa kifungu kisichozidi
miaka mitatu au kulipa faini ya Ksh. Million moja ( sawa na milioni 20 za
Tanzania) kila mmoja.
Kamau
Kuria alikuwa amedai kwamba maandamano ya kila jumatatu ya wafuasi wa Cord
yalikuwa yanatatiza nchi, huku muungano wa Cord nao ukishiikilia kwamba
maandamano hayo yataendelea hadi makamishama wa tume ya uchaguzi watakapoondoka
ofisini.
Maandamano
hayo yamesababisha uharibifu mwingi wa mali na watu sita kupoteza maisha yao.
Aidha, Cord inadai kwamba tume hiyo
ilipendelea serikali wakati wa uchaguzi mdogo wa County ya Kericho na kwamba
hawana imani nayo huku uchaguzi wa uraisi ukitarajiwa kufanyika mwakani.
Mrengo
wa upinzani umesema utatoa taarifa kesho alhamisi kuhusu msimamo wao dhidi ya
maadnamano hayo.
Hata
hivyo serikali na upinzani wamekubaliana kukaa pamoja na kutafuta suluhu, baada
ya viongozi wa kidini nchini Kenya kuingilia kati mzozo huo ambao ulikuwa
unaendelea kushika kasi.
Viongozi
hao wametaka serikali na upinzani utoe wawakilishi saba kila upande kwa
mazungumzo ya kutatua swala hilo.
No comments:
Post a Comment