Thursday, June 16, 2016

RC Mtwara apiga marufuku ujenzi holela.




Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.



Na Juma Mohamed, Mtwara.


MKUU wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amepiga marufuku ujenzi holela katika manispaa ya Mtwara Mikindani ambayo inaelekea kuwa jiji, na kuwataka madiwani kusimamia vizuri shughuli za ujenzi ili wananchi wajue mapema ikiwa wanajenga kinyume na taratibu.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri  hiyo amewaonya madiwani kuacha kuwa mahodari wa kujibu hoja baadala ya kuwa watendaji wazuri kwa maslahi ya halmashauri hiyo na wananchi wao.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.



“Niwaombe watu wa mipango miji na madiwani kuhakikisha mtwara inakuwa kwenye hadhi ya jiji, maeneo ya wazi yawe wazi sitopenda kuona ujenzi holela ukiendelea na ninyi mpo ambapo mwananchi anaanza taratibu za ujenzi hadi anamalizi ndipo mnaenda kumwekea alama nyekundu wakati ananza mlikuwa wapi….. sitopenda kuona hili”,Alisema Dendego. 

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani wakiwa katika moja ya vikao vya baraza.



Aidha, amesema hatopenda kuona hoja zikizaliwa wakati mtu hajakamilisha majukumu yake ambapo wao kama viongozi watekeleze majukumu yao ili kuweka Mtwara katika hatua ya mbele zaidi kimaendeleo kutoka ilipofikia hivi sasa.
Amesema Mtwara inatarajia kupandishwa hadhi kutoka katika mji na kuwa jiji hivyo wamdiwani hao wakiwa kama watendaji na ndiyo wawakilishi wa wanachi wanatakiwa kujipanga kikamilifu kuhakikisha mtwara inafikia kwenye hatua hiyo kinyume na hapo wauangusha mkoa na wananchi kwa jumla.
Naye, mkuu wa wilaya ya mtwara Fatma Ally amewataka madiwani hao kuonyesha ufanisi wao wa kazi hasa katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ili kuhakikisha mapato hayo hayapotei na wao kama madiwani ndiyo watachangia kushuka au kupanda kwa mapato ya halmashauri hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.



“Ni lazima kila kata kujiwekeka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwani ni aibu kuona ninyi wenyewe viongozi mnajenga hoja  kuhusu mapato wakati ndiyo watendaji kwakweli katika hili ni lazima tujipangie malengo mazuri..sipendi kuona wewe kama diwani kwenye kikao unaleta hoja ya mapato..” alisema.
Meya wa manispaa hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao hicho Godfrey Mwanchisye amewataka madiwani hao wawe na moyo wa kujadili masuala mbalimbali na yenye tija ili kujenga halmashauri yao.

No comments: