Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba. |
Juma Mohamed, Mtwara.
Mkuu wa mkoa
wa Mtwara, Halima Dendego ameamrisha kukamatwa na kufikishwa mahakamani
watumishi wanne wa idara ya manunuzi ya halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha wakati wa mchakato wa
tenda ya kutafuta mkandarasi wa ujenzi wa barabara za halmashauri na
kuisababishia halmashaurii hasara ya sh. Milioni 27.
Hatua hiyo
imetokana na hoja ya kutaka kuchukuliwa hatua watumishi hao iliyowasilishwa na
mweka hazina wa halmashauri hiyo Ally Machela, katika kikao maalum cha baraza
la madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na kuungwa mkono na wajumbe wote.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Tandahimba. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tandahimba, Emmanuel Luhahula. |
“Waheshimiwa
madiwani naomba tusifanye kazi kwa woga, nyinyi ndio wenye halmashauri na
nyinyi ndio mliopewa dhamana kwa niaba ya wananchi, mnapoongea na watendaji ni
rafiki zenu pale wanapoenda vizuri, lakini pale wanapoipeleka halmashauri
kinyume na taratibu naomba tusiweke pazia tuchukue hatua..hakuna hata mtendaji
mmoja kati ya hao wakuu wa idara ambaye hajaenda shule..” alisema Dendego.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Namkulya Salum alisema watumishi hao ni pamoja na afisa
manunuzi wa halmashauri Michal Ngajua, afisa mifugo Robert Mwanawima, “lakini
pia kuna mtu mmoja anitwa Musa yuko TANROAD pale (Wakala wa Barabara) na mtu
mmoja ambaye anaitwa Bakari, kwahiyo hao kwa ujumla wake ndio ambao wametakiwa
wakamatwe na hatua za kisheria kama ambavyo mkaguzi ametutaka ziweze
kuchukuliwa..” alisema
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego |
Aidha alisema
miongoni mwa udanganyifu ambao umefanywa na watumishi hao ni kubadilisha
mapendekezo yaliyotolewa na mkandarasi husika kampuni ya Accuracy Constructions
Ltd ya kutaka alipwe sh. Milioni 110 ambaye ilibadilishwa na kuwekwa sh.
Milioni 117.
“Tumepata
hasara nyingine, kulikuwa na watu waliomba kwa bei ndogo ya Milioni 110 lakini
tukawapa watu ambao waliomba kwa bei kubwa ya Milioni 127, maana yake
halmashauri imepata hasara y a sh. Milioni 27 kwasababu mtu wa Milioni 110
tungempa angefanya kazi ile nah ii ni katika suala zima la barabara..” alisema.
Kwamujibu wa
taarifa za mkuu wa wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula ni kwamba tayari watuhumiwa
watatu kati yao wameshakamatwa.
No comments:
Post a Comment