Wadau wa huduma za mawasiliano wakifuatilia somo |
Maboksi ya simu bandia |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Wasimamiaji
wa sheria za mawasilino mkoani Mtwara wametakiwa kuwachukulia hatua haraka watu
watakaobainika kwenda kinyume na kuvunja sheria za matumizi sahihi ya
mawasiliano, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya simu za kiganjani.
Akizungumza katika
ufunguzi wa semina ya siku moja ya kutoa elimu kwa umma juu ya ufahamu wa
rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyoendeshwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, alisema
hakuna sababu ya vyombo vya usalama kuwa na kigugumizi katika kuwachukulia
hatua watakaobainika kuvunja sheria za matumizi ya mawasiliano.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego |
“Lengo la
kusajili simu ni kutaka kutambuana, kudhibiti matukio mabaya na ya kihalifu
pamoja na kuhimarisha hali ya usalama..tunatumia mawasiliano kupotosha habari
na kuleta hali ya mtafaruku kwa wananchi kitu ambacho ni kibaya..” alisema na
kuongeza;
“wasimamiaji
wa sheria, kusiwe tena na kigugumizi tunapoanza kutambuana..jeshi la polisi
lisimame katika kutenda haki ili kudumisha usalama..” aliongeza.
Aidha,
alisema wizi wa simu sasa utakua mwisho kwasababu mtu akiiba haitamsaidia kwani
mwisho wake atakamatwa, huku akiamini baada ya semina hiyo kila mtu ataelimika
juu ya matumizi ya simu.
Akiwasilisha
mada ya kwanza katika semina hiyo, Mhandisi wa mfumo rajisi wa namba za
utambulisho wa simu kutoka TCRA, Imelda Salum, alisema kila simu ya kiganjani
ina namba pekee ya utambulisho ambayo inatambulika kama International Mobile
Equipment Identity ( IMEI) ambayo haifanani na nyingine duniani kote.
Alisema,
namba hiyo inamsaidia mwenye simu katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
usalama wa kifaa chake, kutambulika kwa mamlaka husika na vyombo vya usalama.
Alisema kupitia
namba hizo, inamsaidia mmliki kuweza kutambua kama simu yake ni bandia au laa
iwapo atahakiki kwa kunakili namba hizo ambazo atazipata kwa kuangalia ndani
simu baada ya kuiondoa betri au kwa kubonyeza alama ya *#06# kisha zitajitokeza
tarakimu 15 alafu atazituma kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwenda
namba 15090.
No comments:
Post a Comment