Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Jeshi la
Polisi mkoani Mtwara limemfikisha mahakamani John Venans mkazi wa Kimara jijini
Dar Es salaam, kwa makosa ya kughushi nyaraka mbalimbali na kujaribu kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu, katika benki ya Posta wilayani Masasi mkoani
humo.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Mtwara, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe, mapema leo amewaambia waandishi wa habari kuwa
mtuhumiwa huyo akiwa na nyaraka za bandia alikwenda katika Benki hiyo kwa lengo
la kupatiwa mkopo wa sh. Milioni 9 akitumia majina ya Abel Nchaila, ambaye ni
mwalimu wa shule ya sekondari.
"Akiwa
na nyaraka za bandia alienda katika benki ya Posta tawi la Masasi, kwa ajili ya
kupewa mkopo wa sh. Milioni 9 akijifanya yeye ni mwalimu aitwaye Abel Mrahasi
Nchaila ambaye ni mwalimu wa shule sekondari Mangaki wilaya ya Masasi..aliwasilisha
hizo documents zikiwa na vielelezo vyote pamoja na 'salary slip', barua kutoka
kwa afisa utumishi na barua kutoka kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Mangaki.."
alisema.
Aidha,
Mwaibambe amewataka watumishi wa serikali na taasisi za kifedha kuwa waangalifu
katika kuhakiki nyaraka za watumishi ili kuhepukana na matukio kama hayo ambayo
matokeo yake ni kuisababishia hasara serikali.
"Ni
vyema mtu aneomba mkopo, wahusika 'Bankers' wafanye utafiti je huyo anaeomba
kweli ni mtumishi halali wa serikali?..sio suala la barua ya utambulisho, barua
ya utambulisho kwenye suala la huyu John Venans ina muhuri kabisa wa mkurugenzi
lakini ni fojari, 'signature' fojari.." aliongeza Mwaibambe.
Mtuhumiwa huyo
mwenye umri wa miaka 24 amefikisha mahakamani June 24 na kwamba kesi yake
inatarajiwa kuanza kusikilizwa Julai 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment