Atupele Green akiwa mazoezini msimu uliopta na timu ya Ndanda Fc |
Na Juma Mohamed, Mtwara
MSHAMBULIAJI
Atupele Green ambaye msimu uliopita wa alikipiga kwa mafanikio na klabu ya
Ndanda Fc, amejiunga rasmi na klabu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani kwa mkataba wa
mwaka mmoja.
Mshambuliaji
huyo ameiambia Juma News kuwa, sababu ya yeye kuamua kuachana na Ndanda ni
kutokana na viongozi wa timu hiyo kuchelewa kufanya naye mazungumzo na kwamba
walipoamua kufanya hivyo alikuwa tayari amesha ingia mkataba na Ruvu.
"Wao
kutokuwa kwao haraka kufanya maamuzi ndio imepelekea mimi kusaini JKT
Ruvu..lakini nawashukuru mashabiki wa Ndanda najua walikua pamoja na mimi kwa
kipindi chote lakini ni kawaida kwa mchezaji kuhama nikitolea mfano hata
Christiano Ronaldo aliondoka Machester United akaenda Real Madrid."
alisema.
Alisema
uamuzi huo pia ameangalia mustakabali wa baadae wa maisha yake huku akikiri
kwamba alikuwa akiwindwa pia na vilabu vya Simba na Yanga lakini aliamua
kujiunga na Ruvu kwasababu aliona wanaendana na matarajio yake ya baadae.
"Najua
kuna vitu vingi vitasemwa na maneno mengi yatasemwa, lakini baada ya
kushauriana na watu wangu wa karibu tukakubaliana na kufikia hatua ya mimi
kusaini JKT Ruvu.."alisema.
Atupele
ambaye msimu uliopita aliichezea kwa mafanikio Ndanda Fc na kuweza kuifungia
magoli 10 amekiri kuwa na mipango ya kwenda kucheza kwa majaribio nje ya nchi ambao
alianza nayo kablaya kumalizika ligi kuu msimu uliopita.
Aidha,
alisema atawakumbuka kwa kheri wachezaji wenzake wote ambao alikipiga nao
pamoja katika klabu ya Ndanda pamoja na mashabiki ambao walionesha upendo wa
dhati kwake kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupachika mabao.
Mashabiki wa
Ndanda walisema kuondoka kwa mchezaji huyo ni kutokana na viongozi wa timu hiyo
kutokuwa makini katika harakati za kuwabakisha wachezaji wao kwasababu
walitakiwa kuanza kuzungumza nae kabla ligi haijamalizika.
Atupele Green katika moja ya mechi za Ndanda |
Kwa upande
wake, afisa habari wa Ndanda Fc, Idrissa Bandari, alisema waliwahi kufanya naye
mazungumzo mchezaji huyo lakini hawakuweza kufikia makubaliano na kudai kuwa
inawezekana mazungumzo yao hayakuwa na tija kwake.
"Tulijiandaa
kama timu kwa mchezaji kama yeye ambaye alifanya vizuri katika kikosi chetu
mambo mawili yangeweza kutokea, kuendelea kumshawishi abaki au aende kwenye
timu nyingine kwahiyo tulijiandaa kwa mambo hayo ingawa kitu cha kwanza
hakikuwa kwa yeye kuondoka.." alisema Bandari.
Aliongeza
kuwa mwalimu Malale Hamsini tayari ameshapata mbadala wa Atupele (hakumuweka
wazi) ambaye wanatarajia atakuwa na uwezo kama au zaidi ya Atupele na wakati
ukifika wataweka wazi.
No comments:
Post a Comment