Saturday, June 25, 2016

DC Mtwara apiga marufuku wavamizi wa hifadhi ya barabara.





Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya zoezi la kupanda miti lililoendeshwa na TANROADS katika eneo la manispaa ya Mtwara Mikindani.


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Athuman Kambi, akipanda mti.





Juma Mohamed, Mtwara.

MKUU wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wananchi kuvamia hifadhi ya barabara na kujenga bila mpangilio pamoja na kuweka mabango, na kuwataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoani Mtwara kusimamia vyema agizo hilo.
Akizungumza katika zoezi la upandaji miti lililoendeshwa na Wakala hao pembezoni mwa barabara kuu ya Mtwara-Lindi katika eneo la manispaa ya Mtwara Mikindani, alisema manispaa hiyo inaelekea kuwa jiji hivyo haipendezi kuwa katika hali ya uchafu.

Tupande Miti kupendezesha mji



"Katika mkoa wetu na tunajua Mtwara ndio makao makuu ya mkoa, tunachangamoto kubwa sana ya wananchi kuvamia hifadhi ya barabara.kwahiyo niwaombe sana kuhakikisha kwamba yeyote yule hata awe nani ambaye atajenga jengo lake au ataweka kitu chochote katika hifadhi ya barabara basi tuheabie kama huo ni uchafu na unahitaji kuondolewa.." alisema.
Kwa upande wake, mhandisi wa TANROADS mkoa wa Mtwara, Edward Kortina, alisema lengo la kupanda miti hiyo ni kuunga mkono maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, huku baadhi ya wakazi wa manispaa hiyo wakitoa maoni yao juu ya zoezi hilo lililoshirikisha wanahabari wa mkoani humo.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akipanda mti katika eneo la pembezoni mwa barabara kuu ya Mtwara-Lindi katika eneo la Manispaa ya Mtwara Mikindani.



"Tumekuja katika siku hii ya kupanda miti tukiunga mkonosiku ya mazingira ambayo iliadhimishwa tarehe sita na sisi tukaona tusibaki nyuma ni bora tukaunga mkono kwa kupanda miti ili kuweza kutunza mazingira na hifadhi ya barabara..lengo la kupanda miti ni kwa ajili ya kuweka vivuli kwa watembea kwa miguu pamoja na kupendezesha mji.." alisema EDWARD.

Mwandishi wa Juma News, Juma Mohamed, akipanda miti ambao anaimani hauto kauka.



Naye Salma Kayaga, mkazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, amewapongeza TANROADS kwa kutekeleza zoezi hilo ambalo ni endelevu na kuwashauri wadau wengine wa maendeo kuona umuhimu wa suala hilo.
Jumla ya miti hamsini imepandwa na Wakala huo huku lengo likiwa ni kuboresha hifadhi ya barabara pamoja na kuweka vivuli kwa watembea kwa miguu.
..................................................MWISHO..........................................

No comments: