Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP-Henry Mwaibambe. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
JESHI la
polisi mkoani Mtwara linamshikilia Andrea Machael (28) ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Magumchila wilayani Masasi kwa kosa la kumbaka mototo wa miaka
Minane ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi
Magumchila, na kumsababishia maambukizi ya ugonjwa wa zinaa.
Akzungumza
mkoani hapa, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi
ACP-Henry Mwaibambe, alisema hatua hiyo imetokana na mama mzazi wa mtoto huyo kuamua
kwenda kituo cha polisi kutaka msaada wa kumpeleleza mtoto wake, baada ya
kumwona hatembei vizuri huku akificha kueleza sababu.
“Tarehe 16
mwezi huu wa sita majira ya asubuhi mama yake mzazi alimshtukia huyu mtoto kwa
mwendo wake akaona kama hatembei vizuri, sasa akawa anmbana kwanini yuko vile, yule
mtoto akawa anazubaisha sasa Yule mama akamchukua mtoto na kumpeleka polisi
Masasi, sasa pale polisi tuna dawati la watoto na jinsia wakaanza kumu ‘Interview’
Yule mtoto kwanini yuko vile, mtoto akakiri kuwa alikuwa akifanyiwa vitendo vya
udhalilishaji kwa muda mrefu..” alisema.
Henry Mwaibambe. |
Aidha,
Mwaibambe alisema mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akimpa mtoto huyo fedha sh. 500
hadi 1000 katika kipindi alichokuwa anamfanyia vitendo hivyo, amemsababishia
maambukizi ya ugonjwa wa Kaswende ambao umebainika baada ya kwenda kufanyiwa
vipimo vya afya.
“Tukachukua
jukumu la kumpeleka mtoto hospitali ya serikali ya Mkomaindo tukagundua kwamba
mtoto huyo amefanyiwa vitendo hivyo sana na ameambukizwa maradhi ya zinaa
ambayo ni Kaswende..mtuhumiwa akakamatwa siku hiyo hiyo ya tarehe 16 na
tukampeleka hospitali kwenda kumpima na kweli akagundulika mtuhumiwa ni
mwathirika wa ugonjwa wa Kaswende..” aliongeza.
Alisema,
tayari upelelezi juu ya tuhuma hizo umekamilika ambapo mtuhumiwa huyo ambaye
yuko rumande anatarajiwa kufikishwa mahakamani June 17 mwaka huu huku kesi yake
itasikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Masasi.
Katika hatua
nyingine, Mwaibambe amesema jeshi la polisi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kudhibiti matukio ya wizi ambayo yalijitokeza katika manispaa ya Mtwara
Mikindani yalioambatana na imani za kishirikina.
No comments:
Post a Comment