Salum Minelly, akimiliki mpira mbele ya Juma Jabu wa Kagera Sugar. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
MCHEZO wa
kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mabingwa wapya
Yanga Sc waliopambana na Ndanda Fc, umekuwa ni wa kumfuta machozi kiungo kinda
wa Ndanda, Salum Minelly, ambaye aliifungia timu yake bao la kusawazisha katika
dakika za majeruhi.
Minelly mwenye
umri wa miaka 17 ambaye huu ni msimu wake wa pili kuichezea timu ya Ndanda
katika ligi kuu, aliwahi kutoa machozi uwanjani Nangwanda Sijaona Mtwara katika
mchezo wao dhidi ya African Sports baada ya kupoteza nafasi takribani sita za
wazi.
“Nilikuwa
nasononeka sana, nilishawahi hadi kulia ‘game’ na Kagera (African Sports)
nilikosa magoli zaidi ya sita ile ‘one against one’ nakosa napoteza lakini
sijakata tama nimshukuru Mungu leo nimefunga na tena nimeifunga timu kubwa..”
alisema.
Mchezaji
huyo ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Ndanda kutokana na namna anavyojituma
uwanjani na kutokuwa na moyo wa kukata tama licha ya kuanzishwa kama mchezaji
wa akiba mara kadhaa, msimu huu amekuwa na bahati ya kuanzishwa na pengine kumaliza
dakika zote 90 chini ya mwalimu Malale Hamsini.
Kikosi cha Ndanda Fc. |
Alisema,
ukame wa mabao ambao alikuwa akikabiliana nao haukumkatisha tamaa bali ilikuwa
ni chachu ya kuzidi kuongeza juhudi huku akiamini ipo siku atafunga goli,
pamoja na kuwashukuru wachezaji wenzake na mwalimu wao kuweza kumpa moyo pale
inapotokea anakosa nafasi nyingi za kufunga.
“Walikuwa
wananiambia tu ongeza juhudi utafunga ipo siku utafunga, nashukuru Mungu nimefunga
leo wamenipongeza wote wameniambia tulichokuwa tunakuambia leo kimetokea, nawashukuru
wachezaji wengu wote kwa kunipa ‘support’ yao nashukuru..tuzidi tu kumwomba
Mungu inshaallah kila kitu kitawezekana.” Aliongeza.
Alisema kitendo
cha kufunga katika mechi dhidi ya Yanga ni kitendo cha kufurahisha na kinampa
moyo wa kuzidi kufanya vizuri ikiwa ni goli lake la kwanza la msimu ingawa ligi
imebakiza mchezo mmoja iweze kumalizika, na kudai kuwa anajipanga kwa msimu
ujao.
2 comments:
kila kitu ni mipango....viva ndanda
Yah ni kweli bab..ila dogo anapambana kiukweli, pamoja na ufupi wake lakini anawatoa jasho wapinzani.
Post a Comment