wachezaji wa Ndanda na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo |
Pongezi |
Wachezaji wa Ndanda wakiwasubiri wachezaji wa Yanga waingie uwanjani ili wawapigie makofi |
Wachezaji wa Ndanda wakipongezana baada ya kupata bao la kuongoza |
Na Juma Mohamed, Dar es Salaam.
KUTOKA hapa
uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya
wenyeji Ndanda Fc dhidi ya Yanga imemalizika huku timu hizo zikishindwa
kutambiana baada ya kwenda sare ya magoli 2-2.
Ndanda
walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 28 mfungaji akiwa ni Omary
Mponda kwa mkwaju wa penaiti baada ya mshambuliaji Atupele Green kufanyiwa
madhambi katika eneo la hatari, ambapo bao hilo lilidumu kwa dakika sita kabla
ya Saimon Msuva kuisawazishia Yanga baada ya kuunganisha krosi ya Geofrey
Mwashiuya.
Kipa wa Yanga akijaribu kuufuata mpira wa penalti uliopigwa na Omary Mponda na kuifungia timu yake ya Ndanda bao la kuongoza |
Dakika ya
40, Donald Ngoma aliipatia Yanga bao la pili baada ya kugongeana vyema na
washambuliaji wenzake, na kuifanya Yanga waende mapumziko ikiwa kifua mbele kwa
mabao 2-1.
Kabla ya
kwenda mapumziko, Ndanda walifanya mabadiliko ya mapema baada ya kocha Malale
Hamsini kuamua kumtoa Buruhan Rashid na kumuingiza Salum Minelly.
Mabadiliko
hayo yalizaa matunda kipindi cha pili baada ya Minelly kuisawazishia Ndanda bao
kufuatia shambulizi la kushtukiza langoni mwa Yanga.
Kipindi cha pili
Yanga walifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwinyi Haji, Donald Ngoma na Haruna
Niyonzima na nafasi zao kuchukuliwa na Matheo Damian, Oscar Joshua na Mbuyu
Twite lakini hata hivyo hayakuwa na faida kwao kwasababu mpaka dakika 90
zinamalizika matokeo yalikuwa ni mabao 2-2.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao la kusawazisha |
Kadi za
njano zilitoka kwa wachezaji Kigi Makassy na Azizi Sibo wa Ndanda pamoja na
Kalvin Yondan wa Yanga kwa kucheza madhambi.
Mfungakji wa
bao la kusawazisha kwa Ndanda, salum Minelly, alisema amejiskia furaha kufunga
goli lake la kwanza tangu aanze kucheza ligi kuu na timu yake hiyo lakini zaidi
ni kuifunga timu ya Yanga na kuahidi kuendeleza kufunga katika mchezo mmoja
uliobaki dhidi ya Mbeya City na michezo mingine ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment