Mwandishi wa Juma News, Juma Mohamed, akifanya mahojiano na Mohamed Kilua, nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam. |
Na Juma Mohamed.
SERIKALI
mkoani hapa pamoja na wadau wake wa maendeleo wameshauriwa kushiriki ipasavyo
katika kuhakikisha timu ya soka ya Ndanda Fc iliyopo ligi kuu ya Tanzania Bara
inapata udhamini wa kudumu kuanzia msimu ujao wa mashindano 2016/2017.
Akizungumza
na Nipashe nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa makampuni ya Kilua Steel Company Group,
Mohamed Kilua, alisema wawekezaji waliowekeza mkoani Mtwara wanao uwezo mkubwa
wa kuidhamini timu hiyo lakini lazima uongozi wa mkoa ushiriki kujenga
ushawishi kwao na sio kuacha jukumu hilo kwa viongozi wa Ndanda pekeyao.
“Unapozungumza
uwekezaji ni lazima uongozi wa mkoa ushiriki, kuanzia mkuu wa mkoa, mkuu wa
wilaya, wakurugenzi, mameneja wa mabenki na wengine wa taasisi tofauti wawe
kitu kimoja hilo linawezekana..kwasababu hivi vitu vina ‘level’ unapoongea wewe
au nikiongea mimi ni tofauti na akiongea mkuu wa mkoa, yani kuna ‘level’ Fulani
ni ya kusikika nay a kusikilizwa..” alisema Kilua.
Mohamed Kilua |
Aidha,
alisema timu hiyo inaweza kuwa timu tajiri pengine kuliko zote hapa nchini kwa
kipindi cha mwaka mmoja iwapo mashabiki na wapenda maendeleo wa mkoa wa Mtwara
wataamua kujitoa kwa dhati kuweza kuichangia sh. 20,000 kila siku kwa muda wa mwaka
mmoja kwa kila mtu, ambapo kiasi hicho kitaifanya timu kumiliki zaidi ya sh.
Bilioni 7 kwa mwaka.
Alisema,
kiasi hicho cha fedha kinaweza kuifanya timu kuanzisha miradi mikubwa ambayo
haigharimu pesa nyingi ikiwapo kujenga viwanda vya Viwembe, Pini na hata cha
Plastiki ambacho alisema kinaweza kukagharimu sh. Bilioni 1.2 ujenzi wake.
“Kwahiyo
mkishakuwa na miradi hiyo maana yake tayari kampuni inajiendesha yenyewe yani
timu inabadilika inakuwa kampuni ambayo inajiendesha..kitu cha kwanza ni umoja,
bila hivyo hamuwezi kutoka na umoja sio tu kwa maneno bali kuwe na mapenzi ya
dhati..” alisema.
Kilua na Kambi |
Kilua ambaye
alifikia kuyaeleza hayo baada ya kutembelewa na uongozi wa timu ya Ndand fc
ukiongozwa na mmoja wa wakurugenzi wake Athumani Kambi na katibu mtendaji,
Seleman Kachele, alisema ugeni huo ulikuwa na lengo la kutaka kujadiliana kwa
pamoja namna ya kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na ukata wa
kifedha, ili iweze kuanza msimu ujao ikiwa katika halinzuri.
Alisema,
viongozi hao walimweleza mengi yanayoikabili timu na kuhitaji kusaidiwa ambapo
aliyapokea na kuwaahidi kuwa atayafikisha katika uongozi wa makampuni yake ili
waone namna ya kuweza kuwasaidia huku akiwaagiza kwenda kuaandaa mchanganuo wa
kuomba udhamini (Proposal) na kisha wamkabidhi ili auwasilishe kwa uongozi
wake.
Katibu wa
Ndanda, Selemani Kachele, alimshukuru Kilua kwa mchango wa mawazo alioutoa na
kuonesha utayari wa kushirikiana na viongozi wa Ndanda kutatua changamoto
zinazowakabili na kusema kuwa anaimani yakitekelezwa ipasavyo basi msimu ujao
timu itakuwa katika hali nzuri.
Timu ya
Ndanda inashika nafasi ya Tisa katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
baada ya kucheza mara 29 na kuweza kujikusanyia alama 34 baada ya kupata alama
moja katika mchezo wake uliopita dhidi ya Mabingwa wapya wa ligi hiyo Yanga Sc
kwa kutoa sare ya mabao 2-2 uwanja wa Taifa.
Itamaliza
michezo yake ya ligi kuu msimu huu Mei 22 mwaka huu pale itakaposafiri kuwafuata
Mbeya City katika mchezo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Sokine jijini
Mbeya.
No comments:
Post a Comment