Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akipokelewa na wanawake wajasiliamali wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, alipokwenda kufanya kikao cha kazi kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi. |
"Karibu mama yetu" |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
BAADHI ya
wananchi wa Tarafa ya Mikindani mkoani hapa, wamewalalamikia madiwani wao
kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa kutokana na kutokuwa na umoja na nia ya kuwaletea
maendeleo wananchi kwa madai kuwa hawana utaratibu wa kukutana kupanga mipango
ya maendeleo kwa pamoja.
Akizungumza
mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima dendego, alipofanya kikao cha kazi na
wakazi wa kata ya Jangwani katika tarafa hiyo, Ahmad Mkumilwa, aliwaita
madiwani hao kuwa ni wanafiki na kwamba kama hataki kuwatumikia wananchi wao
waliowachagua wajiuzulu.
“Tarafa ya
Mikindani ina homa ya siasa, madiwani wote Chadema, CCM na CUF hawakutani
wakapanga maendeleo ya Tarafa hii..kwahiyi ninachokuomba waambie kama
tumewachagua kwa ajili ya kutupa maendeleo sisi waje vizuri, kama hawataki
kutupa maendeleo sisi, wajiondoe mapema iwezekanavyo hatuwezi kukaa na wanafiki,
maana ni wanafiki madiawani wa Mikindani, namwambia Lakshari (Diwani wa Jangwani)
na yeyote Yule nakuambia wewe mkuu wa mkoa hawa ni wanafiki hawakutani..”
alisema.
Alisema,
afisa Tarafa anajitahidi kuitisha mikutano kwa ajili ya kujadili mambo ya
kimaendeleo katika tarafa yao lakini madiwani wanamuangusha kutokana na
kutohudhuria, hivyo kumuomba mkuu wa mkoa kuwaambia umuhimu wa kushiriki
mikutano hiyo na kama wana tofauti za kisiasa basi waziondoe kwasababu hazina
tija kwa sasa.
Katika hatua
hatua nyingine, Mkumilwa, alikemea tabia za baadhi ya wakazi wa mji wa
Mikindani ya kutopenda kuwa na vyoo na kuamua kujisaidia katika nyumba za watu
wacheche walionavyo au katika fukwe za bahari, na kuwataka wenyeviti kukemea
vikali na kuhakikisha wakazi wanakuwa na vyoo.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na mmoja wa wakazi wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, baada ya kufanya ziara na kufanya kikao cha kazi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi. |
Mkuu wa
mkoa, alimwagiza afisa tarafa ya Mikindani, Francis Mkuti, kuhakikisha ndani ya
mwezi mmoja kila nyumba inakuwa na choo, ambapo aliahidi kurudi baada ya muda
huo kukamilika kwa ajili ya kukagua utekelezwaji wa agizo lake.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza na wakazi wa kata ya Jangwani katika tarafa ya Mikindani alipofanya kikao cha kazi na kusikiliza kero za wananchi. |
“Hakuna
binadamu hasiyeenda chooni uonge au kweli?..sasa wewe mtu mzima choo huna
unaenda wapi, kinachotakiwa hapa ni kubadilika ndugu zangu zamani mlikuwa
wenyewe lakini sasahivi hiyo pwani yote inalindwa na ndani ya muda mfupi mtaona
hekaheka zake..sasa ndugu yangu ukutwe pale umevua nguo wewe mwanamke mwenzangu
ukutwe pale itakuwaje? Maana yeke pwani yote sisi tunaseti darubini tutakuwa
tunaiona masaa 24..” alisema Dendego.
No comments:
Post a Comment