Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akipokea taarifa ya shule kutoka kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Madimba, Ahmad Kwerendu, halmashauri ya wilaya ya Mtwara. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WANANCHI wa
kata ya Madimba, halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wametakiwa kushiriki
kikamilifu zoezi la kufyatua Matofali lililolenga kutatua changamoto mbalimbali
za miundombinu ya elimu zikiwamo nyumba za walimu na vyumba vya madarasa.
Agizo hilo
limetolewa juzi mkoani hapa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,
alipotembelea katika shule ya sekondari ya Madimba kwa ajili ya kusikiliza na kutatua
kero mbalimbali zinazoikabili shule hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku
tano anayoifanya mkoani mwake.
Mkuu huyo wa
mkoa alimwagiza mwenyekiti wa kijiji cha Madimba, Mohamed Madiva, awahamasishe
wananchi wake ili watekeleze zoezi hilo kwa haraka ili kutatua tatizo la uhaba
wa nyumba za walimu ambalo linawakabili walimu wa shule hiyo ambao wengi wao ni
wageni kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
“Kila kaya
inakukusanyia matofali, wakitaka kufyatua kwa pamoja haya, wakiamua kila
atafyatua atakuleta haya, mwingine atasema sitaki kushika tope nitanunua haya
mradi mnatengeza kipimo ambacho watu wetu wameletewa kutoka halmashauri..sisi
kule mtuachie tutafute bidhaa za viwandani kwa maana ya ‘cement’ na mabati..”
alisema.
Alimtaka
mkuu wa shule hiyo Ahmad Kwerendu, kuwa na tabia ya kufanya vikao na wazazi wa
wanafunzi wa shule vitakavyosaidia kujadili kwa pamoja namna ya kutatua
changamoto zingine ndogondogo kulingana na uwezo wao.
“Zile siku
za ‘graduation’ kwa wale ambao wanamaliza, utawaita wazazi na kuwa nao karibu
lakini hata wewe pia ushiriki shughuli za kule kama vile kwenye ‘Ward C’
(Kamati ya maendeleo ya kata) wewe ni mjumbe..ule ushirikiano utakuwepo, sisi
sasa hivi tumejikita kwenye madawati haya mpaka tarehe 30 mwezi Mei tutakuwa tumemaliza
tatizo la madawati..” alisema.
Naye mwalimu
wa shule hiyo, Herry Joseph, alisema licha ya kuupokea kwa mikono miwili mpango
wa elimu bila malipo ambao unatekelezwa na serikali ya awamu ya tano, bado kuna
changamoto kubwa kwa wanafunzi zaidi ikiwa ni ukosefu wa madawati na vyumba vya
madarasa hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kusomea katika vyumba vya
Maabara.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Madimba halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Ahmad kwerendu, akisoma taarifa ya shule yake mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego alipofanya ziara shuleni hapo. |
“Nawatakia
kila la kheri katika kuitekeleza hiyo ilani, kikubwa madawati yamekosekana kwa
kiasi kikubwa yanaathiri sana namna ya kujifunza kwa wale watoto..” alisema na
kuongeza;
“lakini
mengineyo ni sisite yanayohusu utawala, ninawaombeni sana kwamba sisi
tunaofanya kazi katika maeneo kama haya tofauti na wanaofanya kazi huko
halmashauri, tunaomba tuthaminiane tunavyoleta tatizo kwenye ngazi hizi
zinazofuata chondechodne jaribu kuona kwamba huyu mtu anaeleta tatizo ni kwa
ajili ya kulinda masialahi ya wale watoto wa mahali pale..” aliongeza Herry.
Mkuu wa
shule hiyo, Ahmad Kwerendu, aliomba ushirikiano udumishwe baina ya uongozi wa
shule, jamii pamoja na viongozi wa ngazi za juu ili kuweza kumaliza changamoto
zilizopo.
No comments:
Post a Comment