Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo, Eva Sipryan, akielezea changamoto zinazowakabili shuleni hapo. |
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na walimu katika shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WANAFUNZI wa
shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara,
wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko pamoja na kung’atwa na wadudu
kutokana na kujisaidia maporini.
Wakizungumza
shuleni hapo, wanafunzi hao walisema tatizo hilo ni la muda mrefu na kwamba
linatokana na kukosekana kwa vyoo karibu na mabweni ambapo wanalazimika
kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kujisaidia huku baadhi yao wakiamua
kujisaidia katika mapori yaliyopo nyuma ya mabweni yao.
“Athari
yakwanza kwamfano shuleni kwetu hapa kuna ugonjwa wa kuharisha, muda wa usiku tunapata
shida kwasababu vyoo vipo mbali alafu kuharisha kule kunahitaji kujisaidia kwa
haraka kwahiyo kutoka hapa mpaka kule inakuwa tunapata shida..” alisema Shadia
Mohamed, mwanafunzi wa kidato cha Nne.
Naye, Eva
Sipryan, mwanafunzi wa kidato cha Nne, alisema hali hiyo inawapa tabu sana na
kupeleka baadhi yao kuoga nje ya mabweni yao nyakati za usiku kwa woga kutokana
na umbali uliopo baina ya vyoo na mabweni.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na walimu wa shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo. |
“Muda
mwingine inatulazimu kwenda kuoga nje kule nyuma ya mabweni, kwahiyo kule
vyooni ni mbali sana na mtu mwingine vyoo vipo mbali alafu unamkuta ugonjwa wa
kuharisha kwahiyo muda ule tunajisaidia nyuma ya mabweni kwahiyo inatuathiri
sana na inapelekea kuwaambukiza wengine..” alisema.
Aidha,
alisema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa maji jambo ambalo linapelekea
wananfunzi kukosa kuoga mpaka muda wa siku Tatu hata mabweni kuwa katika hari
ya uchafu.
Alisema,
maji wanapatiwa kwa wiki mara moja ambapo hata hivyo hupatiwa ndoo Moja ambalo
wanatakiwa watumie kwa shughuli zao zote ikiwamo usafi binafsi, kusafisha
mabweni pamoja na usafi wa vyoo.
“Tunagaiwa
ndoo moja tu kwahiyo kufua, kuoga ndoo hiyo hiyo kwahiyo mabweni yanakuwa
machafu na tunatumia wiki nzima..Ndoo hiyo hiyo unafulia na hiyo hiyo
inakusaidia katika kuoga, maana utakuta kama siku mbili tu ndio unaoga alafu
siku nyingine zote unaingia darasani bila kuoga..” aliongeza Eva.
Mwalimu
Mkomo Katani, ambaye husimamia masuala ya afya za wanafunzi shuleni hapo,
aliiomba serikali kuushinikiza uongozi wa shule kuona umuhimu wa kujenga vyoo
karibu na mabweni ili kuhepusha athari za kiusalama kwa wanafunzi pamoja na
kupatwa na magonjwa ya milipuko.
“Lakini siku
ambayo Yule motto akiumwa na Nyoka tutakuja kuambiwa walimu mulikuwa wapi, hali
ya kuwa serikali au uongozi wa shule umeshindwa kutengeneza miundombinu mizuri
wale watoto wakapa vyoo ambavyo itakuwa ni rahisi kwenda kujisaidia..bweni liko
kule lakini vyoo vipo mita 100, sasa motto amebanwa usiku na mkojo au haja
kubwa atashindwaje kwenda kichakani ambako ni karibu kuliko aende choo ambacho
kiko mbali..” alihoji.
Mkuu wa mkoa
wa Mtwara, Halima Dendego, ambae alifika shuleni hapo kusikiliza kero
mbalimbali pamoja na kupokea maoni ya walimu ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya
kutembelea sehemu mbalimbali mkoani hapa, aliutaka uongozi wa shule
kushirikiana na jamii inayowazunguka kutatua changamoto hizo ambazo zipo ndani
ya uwezo wao.
Alisema, sio
kila jambo linatakiwa kuilalamikia serikali, mambo mengine yanatakiwa kumalizwa
na wananchi wenyewe kwa manufaa yao huku yale makubwa ndio yanapaswa kufikishwa
katika ngazi za juu kwa ajili ya msaada zaidi.
“Mtachekesha
sana leo shule kubwa kama hii kuvuna maji tu mpaka mkuu wa mkoa aingilie kati..mimi
nimekaa nina mwaka sasa, lini nimepata hodi ya mkuu wa shule kwamba mkuu mimi
nina mradi huu nina ‘proposal’ naomba tutafutie fedha, mpaka leo nimekuja kama
nisingekuja?..wewe mwenye tatizo umejipanga vipi kulimaliza?..maana katika
mambo yote mliyosema ndugu zangu hakuna jambo kubwa hapa..” alisema Dendego.
Mkuu wa mkoa
anafanya ziara ya kikazi katika halmashauri za Mtwara Mikindani, halmashauri ya
Wilaya ya Mtwara pamoja na halmashauri ya mji wa Nanyamba kwa ajili ya kukagua
miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo anatarajia
kuhitimisha Mei 24 mwaka huu katika halmashauri ya Nanyamba.
………………………………………………mwisho……………………………………………….
No comments:
Post a Comment