|
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli, Amina Mussa, katika maafali ya kuhitimu mafunzo hayo katika ukumbi wa hoteli ya Old Boma.
|
|
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea katika maafali ya kuhitimu mafunzo ya hoteli katika hoteli ya Old Boma, Mtwara.
|
|
Wahitimu wa mafunzo ya hoteli
|
|
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli mmoja wa wahitimu hao.
|
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WAZAZI na
walezi mkoani hapa wametakiwa kuwaendeleza kielimu watoto wao walioishia katika
elimu msingi ili waweze kunufaika na uwekezaji unaofanyika kupitia kampuni
mbalimbali.
Akizungumza
katika maafali ya kuhitimu mafunzo ya hoteli yaliyofanyika katika hoteli ya Old
Boma, Mikindani, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, alisema vijana wengi
wanahangaika kutafuta ajira kutokana na kukosa elimu kwasababu wengi wao wana
elimu ya msingi ambayo haiwezi kuwapatia ajira itakayokidhi mahitaji yao.
Alisema, kwa
namna ambavyo kasi ya uwekezaji inavyoongezeka mkoani hapa ndivyo ambavyo
mahitaji ya ajira kwa vijana yanavyozidi kukuwa, hivyo ni jukumu la wazazi kuona
umuhimu wa kuwaendeleza vijana wao kwasababu kuna vyuo mbalimbali vinavyotoa
fani zitakazowasaidia kupata ajira.
|
Fatma Ally
|
“Kwahiyo
mwanao ambaye ameishia darasa la saba hebu jitahidi ufanye mpango baada ya
miaka miwili hijayo afanye mtihani wa ‘form four’..na yule ambaye amemaliza
‘form four’ asitegemee tu JKT, mfano mimi JKT pale nina nafasi sita za darasa
la saba ambazo inabidi nizigawanye katika halmashauri Tatu..” alisema.
Aliwataka
wananchi wa Mtwara kutokubali kuwa mashuhuda wa maendeleo kwa wenzao kutoka maeneo
mbalimbali kwa kuacha fursa ambazo zinaweza kuwanufaisha zikiwanufaisha wengine
kutokana na kuwa nyuma kielimu.
Aidha,
alilipongeza shirika la Trade Aid ambalo ndio wanaondesha mafunzo hayo kwa
wahitimu katika Hoteli Hiyo ya kitalii iliyopo katika mji wa Mikindani, kwa kushirikiana
na wakazi wa mji huo na kuweza kuendeleza miradi mbalimbali ikiwamo kuendesha
Hoteli hiyo.
|
Kwaito nayo ilihusika kwenye mahali
|
Naye, meneja
mradi wa Shirika hilo Emmanuel Mwambe, alisema shirika lilianza ukarabati wa
jengo la Old Boma mwaka 1999 ambapo lilipata kibali kutoka katika serikali ya
wilaya na miaka mitano baadaye ikafunguliwa hoteli kwa malengo ya kuisaidia
jamii ya wakazi wa Mikindani na Mtwara kwa ujumla.
“Lakini
Trade Aid tukafikiria tukasema hapana tutasaidia vipi, sio biashara ya hoteli,
ngoja tuangalie tunafundishaje vijana amabao wataenda kujiajiri, na kweli Trade
Aid imeanza kutoa mafunzo yake kwa miaka mingi katika fani mbalimbali na mimi
nilikuwepo hapa miaka ya nyuma kama mwanafunzi..” alisema.
|
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli, Amina Mussa, katika maafali ya kuhitimu mafunzo hayo katika ukumbi wa hoteli ya Old Boma.
|
Amina Mussa,
ambaye ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo, alisema amefurahishwa na hatua
kuhitimu kwani baada ya hapo anatarajia kupata ajira kupitia ujuzi wa masuala
ya hoteli ambao ameupata katika kipindi chote cha mafunzo, huku akiwataka
vijana wengine kuchangamkia kujiunga na mafunzo hayo yanayotolewa bila malipo.
|
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa hoteli ya Old Boma na wahitimu wa mafunzo ya hoteli.
|
No comments:
Post a Comment