|
Waandishi wa habari wa Mtwara wakifanya usafi katika eneo litakalojengwa kituo cha Polisi, Msijute, Mtwara
|
|
Waandishi na usafi
|
|
Baada ya kazi, waandishi wakisubiri Chakula
|
|
Waandishi wakisubiri chakula kwa pozi tofauti
|
|
Hatimaye muda wa chakula ukawadia..hapo mwenyekiti wa MTPC, Hassan Simba akijipatia chakula
|
|
Hassan Simba kazini
|
Na Juma Mohamed, Mtwara.
KATIKA
kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (Media Day), Chama cha
Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) kimeungana na baadhi ya wadau wake
kufanya usafi katika eneo linalotarajiwa kujengwa kituo cha polisi lililopo
kijiji cha Msijute jirani na kiwanda cha Saruji cha Dangote Industries Ltd.
MTPC
iliungana na viongozi wa kiwanda hicho, jeshi la Polisi pamoja na viongozi wa
vijiji vyote vinavyozunguka kiwanda cha Dangote katika kutekeleza shughuli hiyo
ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuzikumbusha mamlaka husika umuhimu wa
kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ambacho jiwe la msingi liliwekwa toka mwaka
2014.
|
Waandishi wa Mtwara kazini-Media Day
|
Akizungumza katika
eneo hilo, mwenyekiti wa MTPC Hassan Simba, alisema uamuzi wa shughuli hiyo
kufanyika katika eneo hilo ni kwa ajili ya kulikumbusha jeshi la Polisi na
uongozi wa Dangote ambao ndio ulitoa ahadi ya kujenga kituo hicho kwamba kuna
umuhimu wa kuharakisha ujenzi huo ambao kukamilika kwake kutasaidia kuimarisha
ulinzi na usalama wa kiwanda pamoja na jamii ya vijiji jirani.
“Kuna
umuhimu sasa wa kuharakishwa ujenzi wa hiki kituo hapa, kwasababu sisi tumekuwa
tunazunguka huko mitaani na tunaona wenzetu wa jeshi la polisi wanavyohangaika
kukimbia na vijana wachache ambao sio waaminifu huko mapolini wanaoiba vitu..kwahiyo
tunaamini kituo kikiwa hapa kwao wao itakuwa kazi nyepesi na wataweza kufanya
kazi zao vizuri..” alisema.
Katibu wa
chama hicho, Bryson Mshana, akizungumzia uhuru kwa wanahabari wa Mtwara,
alisema waandishi kwa kiasi kikubwa wamejenga mahusiano mazuri na jamii pamoja
na taasisi mbalimbali zikiwemo za kiusalama ambapo ukiachiliambali baadhi ya
waandishi waliopata misukosuko wakati wa vurugu za gesi mwaka 2013, hakujawahi
kutokea kadhia yoyote kwa waandishi na wadau wao.
|
Katibu wa MTPC Bryson Mshana akielezea jambo
|
“Waandishi
wana uhusiano nzuri na jeshi la polisi na ndio maana tumewashirikisha katika
tukio hili lakini pia Mtwara waandishi hawana tatizo na wawekezaji, wawekezaji
wamekuwa wakitoa ushirikiano na nafikiri kuna taratibu za kufika katika eneo la
uwekezaji kwahiyo wamekuwa wakituruhusu na jeshi la polisi pia..sio kwamba
hatupati misukosuko na jeshi la polisi lakini wamekuwa waki ‘react’ haraka
inapotokea pale mwandishi amepatwa na tukio..” alisema.
Mwakilishi
Mkazi wa Dangote Industries Ltd, Esther Baruti, aliwaondoa hofu wakazi wa
vijiji hivyo na Mtwara kwa ujumla kwa kuwaambia kuwa tayari ramani kwa ajili ya
ujenzi wa kituo hicho imekabidhiwa kwa jeshi la polisi ambao wanasubiri kibali
kutoka makao makuu ili ujenzi uanze.
|
Mwakilishi Mkazi wa Dangote Industries Ltd, Esther Baruti, akiongea jambo
|
“Kwahiyo
naomba majirani zetu na watu wote turudishe ushirikiano uliokuwepo, tusikubali
watu wanaoingia katikati kuvuruga amani ya huku na kitu kingine mkumbuke Alhaj Dangote
alitoa ahadi mbalimbali hizo ahadi atazitekeleza baada ya uzalishaji kukamilika
rasmi, kwasababu sasa hivi bado kiwanda hakijakamilika kipo kwenye majaribio na
bado ujenzi wa ‘power plant’ unaendelea..” alisema.
|
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, George Salala, akieleza jambo
|
Kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Mtwara, George Salala, akizungumza kwa niaba ya kamanda wa
mkoa ACP-Henry Mwaibambe, aliwaashukuru wanahabari kwa kutambua umuhimu wa
kuwapo kwa maendeleo na usalama kwani mambo hayo hayapaswi kwenda tofauti, huku
akiwasifu kwa namna wanavyokuwa wepesi katika kutekeleza majukumu yao na
kushiriki shughuli za kijamii pale inapobidi.
|
Kaimu kamanda wa polisi George Salala akijipatia chakula
|
No comments:
Post a Comment