Tuesday, July 8, 2014

VAN PERSIE AAHIDI KUREJEA KUCHEKA NA NYAVU DHIDI YA ARGENTINA KESHO

Robin Van Persie
Na Juma Mohamed

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uholanzi Robin van Persie bado anasubiri bao lake la kwanza kwenye mechi ya mtoano katika dimba kuu la kimataifa.
Nyota huyo wa Manchester United kupitia bao lake la kichwa la kupiga mbizi alisaidia Uhispania kuanza awamu ya makundi kwa soka ya kupendeza, lakini tangu wakati huo hajawa na mfululizo mzuri wa kupachika mabao mpaka sasa, ambapo kesho Jumatano atakiongoza kikosi cha #theorange katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Argentina.

Baada ya kufunga mabao mawili wakati wa ushindi wao wa 5-1 dhidi ya Uhispania, alifunga wakati wa ushindi wao wa 3-2 dhidi ya Australia, lakini tangu wakati huo, ameenda dakika 225 bila kufunga.
Alisimamishwa mechi dhidi ya Chile, na akaondolewa dakika ya 76 dhidi ya Mexico na kulazimika kutazama mechi kutoka kwenye benchi huku mchezaji aliyechukua nafasi yake, Klaas-Jan Huntelaar, akifunga penalti dakika za mwisho iliyosaidia Uholanzi kusonga.
Robofainali dhidi ya Costa Rica, alishindwa kufunga mara nyingi, moja ikiwa pale kombora lake la dakika za mwisho lilipozimwa kwenye mstari wa goli na Yeltsin Tejeda, kabla yake kufunga wakati wa mikwaju ya penalt.
Mchezaji huyo wa miaka 30 aliongea waziwazi kuhusu hamu yake ya kutaka kua mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya mechi zake za kwanza mbili, lakini kukiwa na mechi mbili zilizosalia, yuko nyuma ya James Rodriguez wa Colombia kwa mabao matatu katika mbio za kutwaa tuzo ya Golden Boot.
Mambo yalivyo sasa, fowadi huyo wa zamani wa Arsenal anaonekana kufuata mtindo ambao umepelekea yeye kufunga mabao yake yote dimba kuu ngazi ya makundi.
Katika kila fainali za Kombe la Dunia alizocheza awali,  2006 na 2010, alifunga bao moja pekee katika raundi ya kwanza, na kukosa kuongeza idadi ya mabao aliyofunga Afrika Kusini miaka minne iliyopita licha ya kuanza katika kila mechi licha ya Uholanzi kufika fainali.

Katika Euro 2008, alifunga mawili katika ngazi ya makundi, lakini Uholanzi walishindwa na Urusi robofainali, na katika Euroo 2012 alifunga bao moja na timu yake ikabanduliwa raundi ya kwanza.
Hakuna shaka kwamba alitilia maanani mashindano haya alipotangaza mkesha wa Uholanzi kusafiri Brazil kwamba: “Kombe hili la Dunia halihusu tu Robin van Persie.
"Ni kuhusu timu yetu kufanya vyema,” akaongeza. “Huwa napenda michuano mikubwa, lakini si lazima ning’ae.”
Maandalizi ya Van Persie kwa michuano hiyo yalitatizwa na hali kwamba alikaa nje wiki sita kutokana na jeraha la goti alilopata dhidi ya Olympiakos katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baadaye Machi.
Alianza mechi akichezea United mara moja kabla ya msimu kumalizika na hakutumika mara kwa mara katika mechi za Uholanzi za kujiandaa kwa Kombe la Dunia, akifunga mara mbili – dhidi ya Ecuador na Ghana – lakini aliondolewa mapema katika mechi zote tatu.
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal ameendelea kutahadhari Brazil, akimtoa Van Persie uwanjani katika mechi zake za kwanza tatu, na kwa kuendeleza umoja kwenye timu, nahodha huyo amekuwa akikubali hayo.
"Sisi ni kikosi cha wachezaji 23,” Van Persie alisema. "Hali ni nzuri kabisa. Sina cha kulalamikia.”
Uhusiano mzuri kabisa kati ya Van Persie na Van Gaal, atakayekuwa kocha wa United baada ya Kombe la Dunia, ina maana kwamba hana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu nafasi yake katika timu.

Lakini ingawa tabia ya Argentina ya kushambulia ina maana kwamba huenda akawa na nafasi zaidi ya kutamba kuliko ilivyokuwa dhidi ya Costa Rica waliojilinda sana, anaishiwa na muda wa kufanya mambo ya kukumbukwa katika michuano hiyo mikubwa zaidi ulimwenguni.

No comments: